Pata taarifa kuu
DENMARK-USHIRIKIANO

Denmark yawaondoa wanajeshi wake nchini Mali

Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya ombi kutoka kwa mamlaka ya mpito ya Mali ambao ulitolewa siku ya Jumatatu na kurejelewa siku ya Jumatano Januari 26. Bamako inadai kuwa haikutoa idhini yake kwa kutumwa kwa wanajeshi wa Denmark waliojumuishwa katika kikosi cha kupambana na ugaidi cha Takuba

Denmark ilikuwa imetuma wanajeshi zaidi ya mia moja kutoka vikosi maalum huko Ménaka, kaskazini mwa Mali, kushiriki katika mapambano dhidi ya ugaidi ndani ya kikosi cha Takuba.
Denmark ilikuwa imetuma wanajeshi zaidi ya mia moja kutoka vikosi maalum huko Ménaka, kaskazini mwa Mali, kushiriki katika mapambano dhidi ya ugaidi ndani ya kikosi cha Takuba. © AFP/Thomas Coex
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kujiondoa kwa wanajeshi wa Denmark nchini Mali lilitolewa Alhamisi mchana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Jeppe Kofod. "Denmark imefukuzwa nchini Mali. Hatukubali na kwa sababu hiyo tumeamua kuwarejesha nyumbani askari wetu,” amesema. Waziri wa Mmabo ya Nje wa Denmark anashutumu kile alitochaja kama "mchezo mchafu wa kisiasa" kutoka viongozi wa mapinduzi nchini Mali, wanaotuhumiwa "kutotaka mpango wa haraka wa kurejea kwa demokrasia nchini Mali. "

Maneno haya ya hasira yanakuja kufunga mlolongo wa siku nne ambapo mvutano ulikuwa ukiendelea kuongezeka. Baada ya kuwasili kwa askari zaidi ya mia moja kutoka vikosi maalum vya Denmark huko Ménaka, kaskazini mwa Mali, kushiriki katika mapambano dhidi ya ugaidi ndani ya kikosi cha Takouba, Bamako ilisikitishwa na kutokuwepo kwa makubaliano ya pande mbili kati ya Mali na Denmark.

Copenhagen, kisha nchi kumi na tano za Ulaya zinazochangia askari wanaunda Takouba, zilijibu kwamba kutumwa kwa askari hao ukulifanyika kwa mwaliko wa mamlaka ya Mali na kwa kufuata sheria zilizopangwa. Lakini kufuatia ombi jipya la Bamako la kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa nchi hiyo, Denmark haikusisitiza zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.