Pata taarifa kuu

Zimbabwe yaanza tena kugawa ardhi zilizotelekezwa na wakulima weusi

Zimbabwe imeanza kugawa upya ardhi ambazo hazikutumika na ambazo zilipewa wakulima weusi wakati wa mageuzi ya umwagaji damu ya ardhi yaliyofanywa na rais Robert Mugabe mapema miaka ya 2000, Waziri wa Kilimo Anxious Masuka amesema Jumatano wiki hii.

Mnamo mwaka wa 2000, rais wa zamani Robert Mugabe aliamuru wakulima Wazungu wa nchi hiyo wanyang'anywe kwa nguvu ili kugawa ardhi zao kwa wakulima weusi. Uamuzi huu ulilenga kurekebisha ukosefu wa usawa uliotokana na ukoloni wa Uingereza, lakini kwa hakika, wale walio karibu na mamlaka walikuwa wamefaidika kwa kiasi kikubwa na ugawaji huu.
Mnamo mwaka wa 2000, rais wa zamani Robert Mugabe aliamuru wakulima Wazungu wa nchi hiyo wanyang'anywe kwa nguvu ili kugawa ardhi zao kwa wakulima weusi. Uamuzi huu ulilenga kurekebisha ukosefu wa usawa uliotokana na ukoloni wa Uingereza, lakini kwa hakika, wale walio karibu na mamlaka walikuwa wamefaidika kwa kiasi kikubwa na ugawaji huu. ASSOCIATED PRESS - Tsvangirayi Mukwazhi
Matangazo ya kibiashara

"Wale wanaomiliki mashamba kadhaa, au wale ambao mashamba yao yametelekezwa, wanajiweka katika hatari ya kunyang'anywa," ametangaza. "Ardhi iliyotelekezwa itagawiwa tena kwa wakulima wapya, ambao wako kwenye orodha ya kusubiri iliyoanzishwa tangu mageuzi ya mwisho," ameongeza.

"Zimbabwe haina ardhi ya kilimo isiyo na kikomo," amesema. "Asilimia 99 ya ardhi tayari inakaliwa, na ardhi tunayowagawia wakulima kwenye orodha ya wanaosubiri inachukuliwa kutoka kwa watu weusi, na kugawiwa tena kwa watu weusi".

Mnamo mwaka wa 2000, rais wa zamani Robert Mugabe aliamuru wakulima Wazungu wa nchi hiyo wanyang'anywe kwa nguvu ili kugawa ardhi zao kwa wakulima weusi. Uamuzi huu ulilenga kurekebisha ukosefu wa usawa uliotokana na ukoloni wa Uingereza, lakini kwa hakika, wale walio karibu na mamlaka walikuwa wamefaidika kwa kiasi kikubwa na ugawaji huu.

Wamiliki hao wapya, waliokuwa na mafunzo duni na vifaa duni, walikuwa wameacha maeneo makubwa ya ardhi ya kilimo yakiwa yametelekezwa na nchi sasa inakabiliwa na uhaba wa chakula. Baada ya kuanguka kwa Robert Mugabe mnamo mwaka 2017, mrithi wake, Emmerson Mnangagwa alipitisha mjadala wa mageuzi na kuahidi kuponya majeraha ya mageuzi ya kilimo, hata kuwalipa fidia wakulima walionyang'anywa. Baadhi ya wakulima Wazungu tayari wameruhusiwa kuchukuwa ardhi kupitia ushirikiano wa ndani, Musaka amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.