Pata taarifa kuu

Uganda: ICC kuaanza kusikiliza kesi dhidi ya Joseph Kony

Nairobi – Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita, ICC, hapo jana imethibitisha kuwa itaanza kusikiliza kesi ya uhalifu dhidi ya kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda, Lords Rseistancy Army, Joseph Kony, ambaye amekuwa mafichoni kwa karibu miongo miwili.

Mahakama ya ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwaka 2005 wakiwemo makamanda kadhaa wa juu wa kundi hilo
Mahakama ya ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwaka 2005 wakiwemo makamanda kadhaa wa juu wa kundi hilo Reuters/Stuart Price/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwaka 2005 wakiwemo makamanda kadhaa wa juu wa kundi hilo, linalodaiwa kuteka mamia ya wasichana na wavulana wanaotumikishwa kama wanajeshi na watumwa wa ngono.

Katika tangazo lake, majaji wa mahakama hiyo wamesema watasikiliza kesi yake hata bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ambapo itaanza kusikiliwa Oktoba 15 mwaka huu.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa majaji kuketi kusikiliza kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2002, makosa yaliyofanywa na Kony, yakitajwa kuwa miongoni mwa uhalifu mbaya zaidi dhidi ya binadamu.

Kisheria mahakama hiyo inaweza kuthibitisha mashtaka ya Kony, bila ya uwepo wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.