Kampuni ya gesi na mafuta TotalEnergies yapata pigo baada ya ufadhili kukatwa
Mashirika karibu 60 ya kiraia kutoka nchi mbalimbali zimetaka benki zote na wawekezaji kusitisha ufadhili wa miradi ya gesi na mafuta inayofanywa na kampuni ya kifaransa ya TotalEnergies katika nchi mbali mbali mradi mkubwa ukiwa nchini Uganda.
Imechapishwa:
Mashirika hayo kupitia barua mbili zilizoandikiwa kwa benki na wawekezaji, yanataka wawekezaji kutotoa mikopo au ufadhili wowote unaohusishwa na TotalEnergies, ambayo yanaishtumu kwa kuendelea na agenda ya kuharibu mazingira licha ya pingamizi kadhaa.
Mashirika hayo yanasema miradi ya Total inaenda kinyume na malengo ya kidunia ya kudhibiti viwango vya joto hati nyuzi moja nukta tano.
Shirika moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la FORED ,lilosaini barua hiyo ,linasema mradi wa Uganda litawaathiri moja kwa moja raia wa DRC, ardhi husika imenyakuliwa kwao , utasababisha uvujaji wa mafuta katika ziwa la Albert na matumizi makubwa ya maji .