Pata taarifa kuu

Uganda: Watetezi wa haki wa kibinadamu wakata rufaa kuhusu sheria dhidi ya mashoga

Nchini Uganda, kundi la watu 22 linalojumuisha watetezi wa haki za binadamu na watunga sheria, wamewasilisha rufaa katika mahakama kuu kupinga sheria tata ya ushoga alioidhinishwa mwaka uliopita.

Naibu jaji mkuu wa Uganda na mkuu wa mahakama Buteera, akiwa na majaji wengine watano, wanatoa uamuzi kuhusu malalamishi yaliyounganishwa kupinga uhalali wa kikatiba wa Sheria ya Kupinga Ushoga mjini Kampala Aprili 3, 2024.
Naibu jaji mkuu wa Uganda na mkuu wa mahakama Buteera, akiwa na majaji wengine watano, wanatoa uamuzi kuhusu malalamishi yaliyounganishwa kupinga uhalali wa kikatiba wa Sheria ya Kupinga Ushoga mjini Kampala Aprili 3, 2024. © BADRU KATUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rufaa hii inawasilishwa baada ya mahakama ya katiba mapema mwezi huu kutupilia mabali kesi iliokuwa imewasilishwa  na kundi hilo kupinga sheria hiyo.

Kupitia wakili wao, Nicholas Opiyo, kundi hilo limeelezea kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama hiyo, hususan uamuzi kwamba kuidhinishwa kwa sheria hiyo hakukuwa kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Sheria hiyo inapendekeza adhabu ya hadi kifungo cha maisha jela kwa wale watakaopatikana kwenye mahusdiano ya jinsia moja, pamoja na uwezekano wa makosa ya ushoga kuadhibiwa kifo.

Sheria hiyo pamoja na hatua ya mahakama ya katiba ya mapema mwezi huu, imekashifiwa vikali na mashirika ya haki za binadamu, zikiwemo nchi za magharibi kama Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.