Pata taarifa kuu

Mjumbe wa UN kuhusu Libya Abdoulaye Bathily ametangaza kujiuzulu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Abdoulaye Bathily ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo,naamini kwamba Umoja wa Mataifa hauwezi "kuchukua hatua kwa mafanikio" kusaidia mchakato wa kisiasa mbele ya viongozi wanaoweka mbele  "maslahi yao binafsi dhidi ya maslahi ya taifa.

Abdoulaye Bathily, Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya.
Abdoulaye Bathily, Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya. UN Photo/Yubi Hoffmann
Matangazo ya kibiashara

Amekatishwa tamaa sana na tabia ya maafisa wa Libya, wanaotuhumiwa kwa ubinafsi, Abdoulaye Bathily aliishia kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu jana kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kabla ya kuitangaza jana Jumanne jioni wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa Baraza la Usalama. Baraza ambapo alitoa picha mbaya sana ya hali ya Libya, iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2011.

Mwanahistoria na mwanasiasa huyu wa Senegal aliteuliwa kuwa mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNMIL) mwezi Agosti mwaka 2022, baada ya miezi kadhaa ya nafasi hiyo kubaki wazi kufuatia kujiuzulu ghafla kwa mtangulizi wake Jan Kubis mwezi Novemba mwaka 2021. Juhudi kadhaa za kuleta Walibya pamoja na kuiongoza nchi kuelekea uchaguzi ambao unapaswa kuiondoa Libya katika kipindi cha mpito ambacho kimekuwepo tangu mwaka 2011.

Katibu Mkuu wa UN-  António Guterres
Katibu Mkuu wa UN- António Guterres AP - Salvatore Di Nolfi

Abdoulaye Bathily, amebaini kuwa UNMIL "imefanya juhudi nyingi katika kipindi cha miezi 18 iliyopita chini ya uongozi wake lakini "katika miezi ya hivi karibuni, hali imekuwa mbaya", akilaani "ukosefu wa utashi wa kisiasa na imani nzuri ya viongozi wa Libya ambao wanafurahia kuona hali hiyo. "Inasikitisha sana, kwa sababu nchini Libya leo, idadi kubwa ya watu wanataka kuondokana na mzozo." Lakini "katika mazingira yaliopo, hakuna njia kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kwa mafanikio", na kuona kwamba "hakuna nafasi ya suluhisho la kisiasa".

Wakati wa mkutano wa Baraza, Abdoulaye Bathily alitangaza kuahirishwa kwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano kati ya Libya uliopangwa kufanyika Aprili 28, hadi tarehe ambayo haijabainishwa.

Abdoulaye Bathily amesema kuwa viongozi wa Libya wanaweka mbele masilahi yao zaidi ya masilahi ya nchi.
Abdoulaye Bathily amesema kuwa viongozi wa Libya wanaweka mbele masilahi yao zaidi ya masilahi ya nchi. AFP / Marco Longari

Libya imetumbukia katika machafuko ya kisiasa na kiusalama tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011 kufuatia uasi wa wananchi walioungwa mkono na NATO. Ikiathiriwa na vurugu na migawanyiko.

Nchi inatawaliwa na na serikali mbili zinazokinzana. Moja ikiwa mjini Tripoli (Magharibi) inaongozwa na Abdelhamid Dbeibah na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine katika Mashariki, imejumuishwa na Bunge na inahusishwa na kambi ya Marshal Haftar, ambayo ngome yake iko Benghazi.

Ali Bilali, RFI-Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.