Pata taarifa kuu

Benki ya Dunia na AfDB zimejitolea kufikisha umeme kwa Waafrika milioni 300

Jinsi ya kutoa huduma bora ya umeme kwa Afrika? Swali hili linajadiliwa katika vikao vya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambavyo vinafanyika kwa sasa huko Washington, nchini Marekani. Marais wa Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika wametangaza ahadi mpya: kuunganisha Waafrika milioni 300 kwenye gridi ya umeme ifikapo mwaka 2030.

Barani Afrika, wakazi milioni 600 hawana umeme.
Barani Afrika, wakazi milioni 600 hawana umeme. Pxabay/Free-photo
Matangazo ya kibiashara

Kuna watu milioni 600 katika bara la Afrika ambao hawana huduma ya umeme. Matokeo: uchumi unatatizika kukuza. "Nishati ni kama damu katika mwili wako: inakuwezesha kuishi. Uchumi hukua kwa ajili ya nishati. Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya nishati na ukuaji wa Pato la Taifa. Hakuna uchumi unaoweza kukua gizani,” amesema Akinwumi Adesina, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Benki ya Dunia ilikuwa tayari imetangaza mpango wa kuunganisha Waafrika milioni 100 kwenye gridi ya umeme. Lakini siku ya Jumatano Aprili 17 huko Washington, taasisi hii inataka kwenda mbali zaidi. "Leo, tunaongeza ahadi hii," anasisitiza Ajay Banga, rais wa Benki ya Dunia. Kwa msaada wa matawi yote ya Benki ya Dunia barani Afrika, tunataka kuunganisha watu milioni 250 kwenye gridi ya umeme. "

Idadi ambayo wataongezwa watu milioni 50 waliounganishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Yote hii itakuwa ghali, karibu dola 30 bilioni. Pesa zilizochukuliwa kutoka kwa hazina ya Benki ya Dunia zilizokusudiwa kwa nchi maskini zaidi. Taasisi hiyo pia inataka kushirikisha sekta binafsi na za umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.