Pata taarifa kuu
MVUTANO-DIPLOMASIA

Burkina Faso yawafukuza wanadiplomasia watatu wa Ufaransa kutokana na "shughuli za uasi"

Baada ya kutangaza kuwa "watu wasiofaa" kwa "shughuli za uasi" na mamlaka ya Burkina Faso, wanadiplomasia watatu wa Ufaransa wametakiwa kuondoka nchini Burkina Faso, kulingana na barua iliyoandikwa siku ya Jumanne na kutumwa kwa ubalozi wa Ufaransa. Uhusiano kati ya Paris na Ouagadougou umezorota sana tangu Kapteni Ibrahim Traoré aingie mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi wa Septemba 2022.

Uhusiano kati ya Paris na Ouagadougou umezorota sana tangu Kapteni Ibrahim Traoré aingie mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi wa Septemba 2022.
Uhusiano kati ya Paris na Ouagadougou umezorota sana tangu Kapteni Ibrahim Traoré aingie mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi wa Septemba 2022. AP - Sophie Garcia
Matangazo ya kibiashara

Wanadiplomasia watatu wa Ufaransa, wakiwemo washauri wawili wa kisiasa katika ubalozi wa Ufaransa huko Ouagadougou, wametangazwa kuwa "watu wasiofaa" kwa "shughuli za uasi" na kuagizwa kuondoka Burkina Faso "katika muda wa saa 48 zijazo", kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso.

Wanadiplomasia hawa watatu "wanatangazwa kuwa watu wasiofaa kwenye ardhi ya Burkina Faso, kwa shughuli za uasi", inabaini wizara katika barua iliyoandikwa siku ya Jumanne na kutumwa kwa ubalozi wa Ufaransa huko Ouagadougou, nakala ambayo France 24 na RFI vimepata leo Alhamisi Aprili 18.

Mnamo Desemba 1, maafisa wanne wa Ufaransa - waliodaiwa kuwa maafisa wa ujasusi na mamlaka ya Burkina Faso, mafundi wa matengenezo ya kompyuta kulingana na chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa - walikamatwa huko Ouagadougou, kufunguliwa mashtaka na kisha kufungwa, kulingana na chanzo kutoka Ufaransa.

Leo wako chini ya kizuizi cha nyumbani, kulingana na vyanzo vya usalama nchini Burkina Faso.

Nchini Burkina Faso pekee, vita na wanajihadi vimesababisha vifo vya raia na wanajeshi 20,000 na takriban watu milioni mbili wamekimbia makazi yao tangu mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.