Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: MONUSCO yajiondoa katika kambi yake huko Bunyakiri, Kivu Kusini

Baada ya kufungwa kwa kambi za MONUSCO za Kamanyola, katika eneo la Walungu, na Amsar katika eneo la Kabare, kambi ya Bunyakiri iliyokaliwa tangu mwaka 2004 na wanajeshi wa Pakistani ilikabidhiwa Ijumaa Aprili 19 kwa vikosi vya jeshi vya DRC wakati wa hafla iliyoandaliwa katika sehemu hii ya eneo la Kalehe lililo chini ya mbuga ya kitaifa ya Kahuzi Biega, kilomita 80 kaskazini mwa Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini.

Serikali ya DRC inawataka walinda amani hao wa MONUSCO kuodoka kwa madai kuwa wameshindwa kumaliza makundi ya waasi.
Serikali ya DRC inawataka walinda amani hao wa MONUSCO kuodoka kwa madai kuwa wameshindwa kumaliza makundi ya waasi. AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum katika Bunyakiri, William Basimike

Akiwa ameketi kwenye kiti cha plastiki, Maliyabo Munganga ni mmoja wa viongozi wa kike wa Bunyakiri. Anasifu juhudi za kikosi cha Pakistani na anahutubia Rais Félix Tshisekedi moja kwa moja: "Wamedhibiti usalama kwa sababu tangu kuwasili kwao, kesi za ubakaji zimepungua. Wanapoondoka, nina wasiwasi kwa sababu bado kuna makundi yenye silaha kilomita chache kutoka hapa lakini namuomba Rais Tshisekedi atuhakikishie ulinzi. Tunataka kujisikia kulindwa na serikali yetu ya Kongo, na tunaomba serikali isitusahau. "

Misheni ilianzishwa huko Bunyakiri kwanza kama kambi ya kuhama hama. Mnamo mwaka wa 2016, kituo hicho kilikuwa cha kudumu na walinzi wa amani 80 walitumwa kulinda zaidi ya wakaazi 10,000. Ebrima Ceesay, mkurugenzi wa usaidizi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, anakumbusha kwamba Umoja wa Mataifa hauitupi DRC: “Baada ya kuondoka kwa MONUSCO, mashirika ya Umoja wa Mataifa, yale yanasimamia masuala ya fedha na programu zingine yataendelea kutoa msaada wao kwa mujibu wa mamlaka yao husika lakini usalama na jukumu la ulinzi wa raia ni la serikali ya Kongo. "

Naibu gavana, Marc Malago, na naibu kamanda anayesimamia utawala na usafirishaji wa jeshi la Kongo katika mkoa wa Kivu Kusini, Jenerali Mabosso Jean-Ladis, walipongeza juhudi za kikosi cha Pakistan katika kurejesha amani. Wanathibitisha: serikali ya Kongo itachukua majukumu yake kuhakikisha usalama wa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.