Pata taarifa kuu

Mkuu wa UN kuhusu haki za binadamu Volker Türk amezuru Goma DRC

Mkuu wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Türk amekuwa akizuru Goma, Mashariki mwa DRC ambako amekutana na wakimbizi waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya utovu wa usalama, huku akitoa wito wa usitishwaji wa vita.

 Volker Türk, Mkuu wa UN kuhusu haki za binadamu Tarehe 8 novemba 2023, alipozuru Rafah Misri.
Volker Türk, Mkuu wa UN kuhusu haki za binadamu Tarehe 8 novemba 2023, alipozuru Rafah Misri. © KHALED DESOUKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuwatembelea raia waliotoroka makazi yao mkoani Ituri lakini pia kambi ya Bulengo yenye raia zaidi ya laki tatu kando ya mwa mji wa Goma Kivu kaskazini, alieleza kuwa UN utafanya Kila juhudi za kuwaajibisha watu wote wanaotatiza usalama wa raia mashariki mwa Congo.

" Kwa hivyo ni wazi kuwa ulinzi wa raia ni kipaumbele cha kila mtu na tunawajibu wa kuhakikisha hivyo wakati kuna vita.Na ni wazi kwamba hali ni mbaya sana, lazima tupigane nayo.” alisema Volker Türk.

00:13

Mkuu wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Türk

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa pia alisisitiza umuhimu wa kuwalinda raia akisema, ni jambo la kipaumbele, akielezea haja ya kufanyia kazi sababu za msingi za migogoro inayowasukuma wakazi kukimbia makazi yao ya awali.

Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya Bulengo, walikuwa na kauli hii baada ya kukutana na Volker Turk.

“Tumechoshwa na maisha ya kuomba omba ,tumedharauliwa na tunaishi katika mazingira magumu sana.” alieleza mmoja wa wakimbizi.

00:15

Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya Bulengo

Itakumbukwa kuwa Volker Turk afanya ziara rasmi DRC ,Siku chache tuu ,baada ya naibu mwakilishi maalum anayesimamia ulinzi na uendeshaji wa jeshi la kulinda amani Umoja wa mataifa MONUSCO, Vivian Van de Perre kufanya ziara mashariki mwa Congo ambapo , alithibisha pia kuunga mkono raia na Serikali ya DRC.

CHUBE NGOROMBI GOMA  RFI- KISWAHILI

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.