Pata taarifa kuu
MAREKANI-CIA-AFGHANISTAN-IRAQ-HAKI

Ripoti kuhusu uovu uliotekelezwa na CIA

Ripoti iliyotolewa na Kamati ya Baraza la Senate nchini Marekani, imeshtumu idara ya Ujasusi nchini humo CIA kwa kuwatesa washukiwa wa ugaidi baada ya mashambulizi ya kigaidi kutokea nchini humo mwaka 2001.

Rais Barack Obama akiwa pamoja na mtangulizi wake George W Bush, ziarani Dar es Salaam, tanzania, mwaka 2013.
Rais Barack Obama akiwa pamoja na mtangulizi wake George W Bush, ziarani Dar es Salaam, tanzania, mwaka 2013. AFP PHOTO / Saul LOEB
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo yenye kurasa zaidi ya elfu sita, imesema washukiwa 100 waliteswa na maafisa wa CIA kati ya mwaka 2001 na 2009 na baadhi ya mateso hayo yalikuwa ni pamoja na kuvuliwa nguo na kumwagiwa maji baridi, kufungiwa kwenye chumba chenye giza, kupigwa na kunyimwa usingizi kwa kipindi kirefu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Senate iliyokuwa inachunguza utendaji kazi wa idara hiyo, Dianne Feinstein, amesema mbinu hizo hazikusaidia kupata taarifa muhimu kuhusu ugaidi kutoka kwa washukiwa na baadhi yao walipoteza maisha, na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa CIA kutorudia mbinu hizo.

Rais Barrack Obama amesema mbinu hizo zilizotumiwa na CIA ni kinyume na sera za Marekani na kuongeza kuwa mbinu hizo zisitumiwe tena katika siku zijazo.

Usalama umekua umeimarishwa katika idara mbalimbali za serikali ya Marekani nchini humo na kwingineko duniani hasa balozi zake , wakati ambapo Baraza la Senate limekua likijiandaa kutoa ripoti hiyo kuonesha namna maafisa wa CIA walivyowatesa washukiwa mbalimbali wakati wa uongozi wa rais George W Bush.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.