Pata taarifa kuu
MAREKANI-NEW YORK-MAANDAMANO-Usalama

Meya wa New York atuhumiwa na polisi

Tangu kuuawa kwa maafisa wawili wa polisi Jumamosi 20 mwaka 2014 katika mji mdogo wa Brooklyn, mkuu wa mji wa New York ameendelea kukusolewa na polisi katika mji huo.

Mkuu wa mji wa New York, Bill de Blasio katika mkutano na vyombo vya habari baada ya vifo vya askari polisi wawili waliuawa Jumamosi katika mji wa Brooklyn, New York tarehe Desemba 22 mwaka 2014.
Mkuu wa mji wa New York, Bill de Blasio katika mkutano na vyombo vya habari baada ya vifo vya askari polisi wawili waliuawa Jumamosi katika mji wa Brooklyn, New York tarehe Desemba 22 mwaka 2014. REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Polisi inamtuhumu mkuu wa mji wa New York kwamba hakuiunga mkono wakati wa maandamano ya raia wakipinga unyanyasaji unaodaiwa kutekelezwa na baadhi ya askari polisi.

Kwa sasa polisi ndio inadai kuwa imekua ikishambuliwa, baada ya hivi karibuni raia kudai kuwa wamekua wakinyanyaswa na polisi. Mauaji ya kikatili ya askari polisi hao yamezua hasira kwa upande wa polisi wa mji wa New York.

Kiongozi wa chama cha askari polisi, amemshtumu mkuu wa mji wa New York, Bill de Blasio, kuhusika katika vifo vya askari polisi hao. Askari polisi wanamtuhumu pia Bill de Blasio, kuchangia kwa kuchochea vurugu kupitia kauli zake ambazo ziliendelea kukuza chuki na kusababisha kushambuliwa kwa polisi.

Bill de Blasio, ambaye ni mume wa mwanamke raia wa Marekani mwenye asili ya kiafrika, alikua akitoa nasaha ya kuwa na huruma zaidi kwa waandamanaji ambao wamekua wakipinga dhidi ya kuachiwa huru kwa afisa wa polisi aliye husika katika kifo cha Eric Garner, raia wa Marekani mwenye asili ya kiafrika aliye fariki baada ya polisi kutumia nguvu zaidi kwa kumkamata katika majira ya joto.

Bill de Blasio amezitaka pande zote husika hasa waandamanaji kusitisha harakati zao, hadi baada ya mazishi ya askari polisi hao wawili waliouawa. Amezitaka pia pande husika kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kuboresha maridhiano kati ya raia weusi  Wa Marekani na polisi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.