Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-MAREKANI-USALAMA

Ufaransa mbioni kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya IS

Moscow inatuhumiwa na Washington kuimarisha uwepo wake wa kijeshi nchini Syria. Kwa mujibu wa Pentagon, katika siku za hivi karibuni, ndege za Urusi zimekua zikibeba vifaa vya kijeshi katika mji wa Latakia, ngome kuu ya rais wa Syria. Silaha hizo zimeonekana pia katika uwanja wa mapambano.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa,  Jean-Yves Le Drian.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian. Reuters/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Vifaru saba vya Urusi vimeonekana kwa satelaiti ya Marekani. Marekani inakaribishwa juhudi za vita za Urusi dhidi ya wanajihadi, lakini inautazama kwa jicho la ubaya msaada wa Urusi kwa Bashar Al Assad.

"

Vifaru vya Urusi, wakati wa kuwasilisha vifaa vya kijeshi karibu na mji wa Moscow, Juni 16, 2015.
Vifaru vya Urusi, wakati wa kuwasilisha vifaa vya kijeshi karibu na mji wa Moscow, Juni 16, 2015. AFP PHOTO / VASILY MAXIMOV

Tunapongeza mchango wa Urusi katika juhudi za vita dhidi ya serikali ya kundi la Islamic State, lakini michango inayoendelea kuusaidia utawala wa Assad, hasa juhudi za kijeshi hawana hazisaidii lolote na zinaweza kuzorotesha zaidi hali ya usalama ", amesema msemaji wa Pentagon, ambaye ametangaza kuwa vifaru saba vya Urusi aina ya T-90 vimeonekana katika uwanja wa ndege kaskazini mwa Syria. Tangu kuanzisha mashambulizi yake ya anga nchini Syria dhidi ya kundi la Islamic State, Marekani kama nchi nyingine za muungano wa kimataifa zinazotoa mchango wao katika nchi hiyo, zinamsaidia, kwa kweli, Bashar Al Assad.

Lakini katika hali halisi kile kinachoitia wasiwasi Washington siyo silaha hizo za Urussia zilizotolewa kwa serikali ya Syria, lakini uwezekano wa kupelekwa kwa askari katika uwanja wa vita nchini Syria. Jeshi la Marekani linaamini kwamba Urusi imekua ikitayarisha kambi ya wanajeshi wake nchini Syria, ikiwa na uwezo wa kupokea waanajeshi 1,500.

Kwa mujubu wa afisa wajeshi la Marekani uwezekano wa kuingilia moja kwa moja wa majeshi ya Urusi katika mgogoro wa Syria unaweza kuhatarisha mwongozo wa operesheni za anga zinazoendeshwa na muungano. Moscow imefutilia mbali shutuma hizo. Hakuna hata askari wao aliyeingia nchini Syria, Maafisa wa Urusi wamesema. Hata hivyo Urusi ilikubali hivi karibun kwamba ilimtumia silaha Bashar Al Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.