Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-USHIRIKIANO

Netanyahu aunga mono suluhu kati ya Marekani na Israel

Barack Obama na Benjamin Netanyahu wamekutana kwa mazungumzo Jumatatu wiki hii mjini Washington. wawili hao walikua hawajazungumza tangu mwezi Julai, na ziara ya mwisho ya Binjamin Netenyahu katika Ikulu ya White House ilikuwa mwezi Oktoba 2014.

Rais wa Mrekani Barack Obama na Waziri mkuu waIsrael Benjamin Netanyahu wakizungumza katika Ikulu ya White House, Washington Machi 12, 2012.
Rais wa Mrekani Barack Obama na Waziri mkuu waIsrael Benjamin Netanyahu wakizungumza katika Ikulu ya White House, Washington Machi 12, 2012. Reuters / Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Barack Obama na Benjamin Netanyahu wameonekana kuweka "kando tofauti zao" kuhusu Iran, kulingana na maneno ya rais wa Marekani. Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel wamezungumzia tu masuala ya wakati huu.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa amefanikiwa kuondoa tofauti zilizo kuwepo kati ya Marekani na Israeli kuhusu makubaliano ya kinyuklia wa iran baada ya kukutana na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Washington jumatatu wiki hii.

Barack Obama ameomba hatua madhubuti ili kupunguza mvutano kati ya Wapalestina na Waisrael. "Nataka kuwa wazi kabisa: tunalaani kwa maneno yenye nguvu mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya raia wasio na hatia wa Israel. Pia nitajadili pamoja na Waziri Mkuu nini anachofikiria kwa kupunguza uhasama kati ya Waisrael na Wapalestina, ni jinsi gani ya kuweza kupata njia ya amani. Na jinsi gani ya kuweza kuhakikisha kwamba matarajio halali ya Wapalestina yanafikia kwa njia ya kisiasa, huku kukiwa na uhakika kwamba Israel inalinda usalama wake ", rais wa Marekani ametangaza mapema Jumatatu wiki hii.

Benjamin Netanyahu amesisitiza kuzingatia binafsi mchakato wa amani ambao ungeweza kupelekea kuundwa kwa taifa la Palestina. Mchakato ambao umesitishwa kwa miezi kadhaa sasa. "Nataka kuwa wazi, hatukukata tamaa ya amani. Mimi ninabaki katika mtazamo wa amani, nchi mbili zenye makundi mawili ya watu :Taifa la Palestina lisilokuwa na jeshi ambalo linatabua taifa la Kiyahudi. Hakuna mtu anatakiwa kuwa na shaka kwa uamuzi wa Israel kujilinda dhidi ya ugaidi, lakini pia hakuna mtu atakua na shaka ya nia ya Israeli ya kudumisha amani na majirani zake, kama kweli wanataka amani. Natarajia kujadili na wewe, hatua madhubuti ambazo zitapunguza mvutano, kuongeza utulivu, na maendeleo ya kupatikana kwa amani",amesema Waziri Mkuu wa Israel.

Waziri Mkuu wa Israel hakika ana hamu ya kuboresha sura yake kwa Marekani. Benjamin Netanyahu atazungumza leo Jumanne jioni mbele ya kundi la wazee wa Busara ambalo ni kama mwanasheria wa makubaliano ya nyuklia ya Iran. Atakutana pia na wabunge kutoka chama cha Democratic ambao waliona walisononeshwa na misimamo hiyo kuhusu suala hilo la nyuklia ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.