Pata taarifa kuu

Trump atoa dola milioni 175 zilizoombwa na mahakama na kupepuka kukamatwa kwa mali yake

Donald Trump amewasilisha dhamana ya dola milioni 175 kwa mahakama za Marekani siku ya Jumatatu jioni, akiepuka matarajio ya kufedhehesha ya kukamatwa kwa mali yake baada ya kukutwa na hatia ya kulipa faini ya dola milioni 454 kwa udanganyifu wa kifedha mnamo mwezi wa Februari, kulingana na hati ya mahakama iliyotolewa hadharani.

Donald Trump anasubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi yake katika mahakama ya New York, Alhamisi, Februari 15, 2024.
Donald Trump anasubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi yake katika mahakama ya New York, Alhamisi, Februari 15, 2024. © Jefferson Siegelon Siegel / AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Marekani, mgombea urais katika uchaguzi ujao, alikuwa na hadi siku ya Alhamisi kutuma dhamana hii iliyofunikwa na kampuni ya bima na ambayo ni sawa na amana, katika kesi hii ya madai ambayo alikata rufaa.

Dhamana hii inampa ahueni, wakati atasikilizwa mahakamani Aprili 15, kwa mashtaka ya jinai wakati huu, katika kesi ya malipo ya siri ili kuficha mambo ya aibu mnamo mwaka 2016, ikiwa ni tukio la kwanza la kihistoria kwa rais wa zamani wa Marekani.

Mahakama ya Rufaa ya New York ililegeza shinikizo la kifedha kwa bilionea huyo wa chama cha Republican mwenye umri wa miaka 77 wiki moja iliyopita kwa kupunguza dhamana katika kesi ya madai kuwa milioni 175.

"Ninaheshimu sana uamuzi wa mahakama ya Rufaa na nitaweka dola milioni 175 (...) haraka sana, ndani ya siku kumi", alijibu mgombea urais kwa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba, ambaye aliongeza mashambulizi makali dhidi ya majaji wake katika kesi ambazo anashitakiwa.

Donald Trump alihukumiwa katikati ya mwezi wa Februari kulipa hadi dola milioni 454 kwa faini na wanawe Eric na Don Jr., kwa udanganyifu wa kifedha ndani ya kampuni yao ya Trump Organization. Walishutumiwa kwa kuingiza mali isiyohamishika yao, kama vile Trump Tower au jengo la 40 Wall Street huko New York, hadi kufikia dola bilioni kadhaa katika miaka ya 2010 ili wapewe mikopo mikubwa zaidi. Baada ya kuhukumiwa, Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la New York Letitia James alitishia kutmia utaratibu wa sheria kukamata mali hiz ili kurejesha thamani ya faini hiyo, akitoa mfano wa jengo la 40 Wall Street.

Hata hivyo Donald Trump bado anakabiliwa na kesi zingine nne, ambazo bado ziko mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.