Pata taarifa kuu
KEA KASKAZINI-Majaribio

Korea Kaskazini imetekeleza majaribio ya zana zake za nuklia

Korea Kaskazini imefanya majaribio ya zana zake za vita karibu na mpaka wake na Korea Kusini, bila hata hivo kusababisha hasara. Majaribio mengine yanasubiriwa mchana wa leo.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akikagua kikosi cha wanajeshi  kisini magharibi mwa nchi.
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akikagua kikosi cha wanajeshi kisini magharibi mwa nchi. © Reuters/KCNA
Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini ilifanya majaribio kama hayo machi 31, ambapo baadhi ya makombora yalidondoka kwenye eneo la bahari la Korea kusini.

Wakati huo Korea Kusini ilijibu kwa silaha nzito nzito.

Hali hio haikusababisha hasara yoyote, bali kulikua na hali ya taharuki kati ya mataifa hayo mawili, baada ya Korea Kaskazini kutangaza kwamba itafanya majaribio mengine ya zana zake za nuklia.

Majaribio ya leo yalidumu dakika 10, huku makombora 50 yakiwa ndio yalifyatuliwa. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini amesema kwamba hakuna kombora hata moja ambalo liliyodondoka kwenye ardhi ya Korea Kusini.

Hili litakuwa jaribio la pili ndani ya mwezi mmoja kutekelezwa na Pyongyang, majaribiuo ambayo yamesalia kuwa hataro kwa usalama katika eneo la Korea.

Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini inasema majaribio hayo yatafanyika karibu na visiwa viwili magharibi mwa eneo hilo la Korea, na jeshi lake liko tayari kwa lolote.

Pyongyang na Seoul zimekuwa zikizonania mpaka karibu na visiwa hivyo ambao uliwekwa na Umoja wa Mataifa baada ya vita vya Korea Kusini na korea Kaskazini lakini hadi sasa pyongyang inakataa kuutambua mkoa huo.

Mwezi uliopita, nchi zote mbili zilirushiana makaombora katika majaribio ya zana zake za kivita.

Mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini.
Mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini. REUTERS/Lee Jong-kun/Yonhap

Jumuiya ya Kimataifa imeendelea kuitenga Korea Kaskazini na kuiwekea vikwazo kwa kuendelea kujaribu silaha zake za Nyuklia, majaribio ambayo mataufa ya Mgaharibi yanasemsas yanatishai usalama wa Mtaufa jirani ambayo ni washirika wake kataika korea Kusini na Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.