Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-UINGEREZA-Maandamano-Siasa

Maandamano yasitishwa Hong Kong

Waanzilishi wa vuguvugu linaotetea na kuunga mkono uwepo wa mfumo wa demokrasia Hong Kong (Occupy Central), wametangaza kwamba watajielekeza Jumanne Desemba 2 kwenye makao makuu ya polisi na wamewataka wafuasi wao kusitisha maandamano.

Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wazuia barabara iliyojengwa aridhini katika mji wa Hong Kong, Desemba 1, 2014.
Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wazuia barabara iliyojengwa aridhini katika mji wa Hong Kong, Desemba 1, 2014. REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano kati ya waandamanaji hao na polisi yaliyotokea Jumapili na Jumatatu Decemba 1 yalisababisha watu 58 kujeruhiwa, wakiwemo askari polisi 11. Na wengine wengi walipata"majeraha madogo," kwa mujibu wa washiriki.

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi Hong Kong, Desemba 1.
Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi Hong Kong, Desemba 1. REUTERS/Bobby Yip

Haijafahamika iwapo ni mwisho wa maandamano ya vuguvugu hilo au wataendelea na maandamano hadi madai yao yapatiwe ufumbuzi.

Waandaaji wa maandamano hayo ambao walikua wakishikilia majengo ya serikali, walibaini Jumamosi Novemba 29 mwaka 2014 kwamba jitihada zao za kuishinikiza serikali kutekeleza madai yao zimegonga mwamba, na kuchukua uamzi wa kusitisha maandamano. Hata hivyo wamepanga kujielekeza Jumanne Desemba 2 kwenye makao makuu ya polosi.

Waanzilishi wa vuguvugu hilo Occupy Central, wamewatolea wito wafuasi wao kusitisha maandamano.

“ Wakati ambapo tukijiandaa kujielekeza kwenye makao makuu ya polisi tunawatolea wito wafuasi wa Occupy Central kusitisha harakati”, amesema Benny Tai, mmoja kati ya waanzilishi wa vuguvugu linalounga mkono mfumo wa demokrasia Hong Kong.

Benny Tai, Chan Kin-man na Chu Yiu-ming waliunda vuguvugu hilol Occupy Central mwanzoni mwa mwka 2013 wakidai kuwepo kwa mfumo wa demokrasia Hong Kong.

Hayo yakijiri ujumbe wa wabunge wa Uingereza wamekataliwa na serikali ya China kuingia Hong Kong.

Mmoja kati ya waandamanaji Hong Kong, Septemba 28.
Mmoja kati ya waandamanaji Hong Kong, Septemba 28. REUTERS/Tyrone Siu/Files

Mkuu wa ujumbe wa Wabunge wa uingereza, Richard Ottaway, amepinga hadharani kupitia vyombo vya habari uamzi huo wa China wa kuwazuia kuingia Hong Kong. Richard Ottaway amesema hiyo ni dhulma wanayofanyiwa na serikali ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.