Pata taarifa kuu
YEMENI-USALAMA-SIASA

Rais wa Yemen aliye uhamishoni arejea Aden

Rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi aliye uhamishoni amewasili Jumanne hii katika mji wa Aden, ziara yake ya pili tangu kuanza kwa vita mwezi Machi mwaka huu, ili kuunga mkono vikosi vinavyoendelea kumtii, afisa kwenye Ikulu ya Yemen ametangaza.

Rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi amerejea nchini mwake kuungana na wanajeshi wanaomtii (picha), hapa ni katika mji wa Taiz, Novemba 16, 2015
Rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi amerejea nchini mwake kuungana na wanajeshi wanaomtii (picha), hapa ni katika mji wa Taiz, Novemba 16, 2015 REUTERS/Anees Mahyoub
Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo Mokhtar al Rahbi, ameeleza kuwa Abd Rabbo-Mansour Hadi amerejea nchini mwake ili kusimamia kampeni ya kijeshi inayolenga kuudhibiti upya mji wa Taiz, eneo kunakoshuhudiwa mapigano makaliambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu zaidi 1,600, kwa mujibu wa tathmini iliotolewa na vyanzo vya hospitali.

"Rais Hadi atakutana na viongozi wa kijeshi ili kufanya tathmini ya hali ya usalama na kusimamia kuingizwa kwa raia wanaopambana upande wa majeshi katika jeshi na vikosi vya usalama", Mukhtar al Rahbi amesema.

Haikuwezekana mara moja kujua ni muda gani Hadi anapania kukaa katika mji huo au ziara yake hiyo katika mji wa aden inaashiria kurudi kwa serikali yake ilio uhamishoni, mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia.

Yemen inakabiliwa na vita kati ya wanamgambo wa Kishia wa Huthi ambao wanabaki wanatawala sehemu kubwa ya nchi hiyo na wanajeshi wanaomti Rais Abd-Rabbou Mansour Hadi, anaye ungwa mkono na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, muungano ambao uliurejesha kwenye himaya ya serikali mji wa Aden mwezi Julai mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.