Pata taarifa kuu
YEMEN-IS-USALAMA

IS yakiri kutekeleza shambulizi la bomu Aden

Kundi la Islamic State nchini Yemen linadai kuwa ndilo lililotekeleza shambulizi la bomu katika kambi ya wanajeshi wa Kimataifa mjini Aden na kusabisha vifovya wanajeshi 15 Jumanne wiki hii.

Moshi kutoka hoteli al-Qasr katikamji wa Aden, Oktoba 6, 2015, kufuatia mashambulizi yaliyonadaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State.
Moshi kutoka hoteli al-Qasr katikamji wa Aden, Oktoba 6, 2015, kufuatia mashambulizi yaliyonadaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter limetoa madai hayo na pia kuweka picha za shambulizi hil dhidi ya vkosi vya Kimataifa wanavyopambana navyo.

Islamic State imesema walipoteza wapiganaji wao wanne baada ya kutekeleza shambulizi hilo ambao imeongeza kuwa wote ni raia wa Yemen.

Wanajeshi 11 wa Yemen na wanne kutoka nchi za Mmiliki za kiarabu waliuawa katika shambulizi hilo kubwa kuwahi kuwalenga wanajeshi wa serikali na wale wa kigeni.

Kuanzia mapema mwaka huu wanajeshi wa Yemen wakisaidia na wale wa Kimataifa wakiongozwa na Saudi Arbaia wamekuwa wakipambana na waasi wa Kihouthi nchini humo.

Watu zaidi ya elfu 4 wamepoteza maisha na maelfu kukimbia makwao kutokana na machafuko yanayoendelea katika nchi hiyo.

Hayo yakijiri maafisa wa usalama nchini Yemen wamesema Waziri mkuu wa nchi hiyo Khaled Bahah amenusurika kifo baada ya hoteli aliokuwa akiishi pamoja na baraza lake la mawaziri kushambuliwa katika mji wa Aden.

Msemaji wa serikali nchini Yemen, Rajeh Badi amewaambia wandishi wa habari kwamba mabomu Kadhaa yalirushwa katika maeneo matatu kutoka nje ya mji huo. Rajeh Badi ameongeza pia kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari.

Milipuko kadhaa ilikumba hoteli ya Qasr siku ya Jumanne asubuhi pamoja na makao makuu ya vikosi vya milki za kiarabu vinavyounga mkono serikali pamoja na nyumba moja.

Vyombo vya habari kutoka Umoja wa falme za Kiarabu UAE vimesema kuwa takriban wanajeshi 15 wa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia pamoja na wapiganaji walio watiifu kwa serikali ya Yemen waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.