Pata taarifa kuu
BANGLADESH

Bangladesh: Ishirini na tano waangamia baada ya meli mbili kugongana

Takriban watu 25 wamepatikana wamefariki Jumatatu hii asubuhi baada ya melimbili kugongana kwenye Mto Padma katikati mwa Bangladesh, polisi imesema.

Ajali za baharini hutokea mara kwa mara nchini Bangladesh, nchi yenye mamia ya mito
Ajali za baharini hutokea mara kwa mara nchini Bangladesh, nchi yenye mamia ya mito AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tumeokoa watu watano na tumepata miili 25," mkuu wa polisi wa eneo hilo Miraz Hossain ameliambiashirika la habari la AFP baada meli iliyokuwa na abiria wasiopungua 30 kugongana na meli nyingine kwenye Mto Padma karibu na mji wa Shibchar. Maafisa wa kikosi cha Zima moto na wenyeji wanaendelea na shughuli za uokoaji, wakati kulingana na vyanzo mbalimbali, watu wengine hawajulikani waliko.

Ajali za baharini hutokea mara kwa mara nchini Bangladesh, nchi yenye mamia ya mito. Wataalam wanasema sababu za ajali hizo ni kutokana na utunzaji duni wa meli, viwango visivyoeleweka katika utengenezaji wa meli, lakini pia wingi wa watu wanaosafiri.

Mapema mwezi aprili, zaidi ya watu 3 waliangamia baada ya kivuko kilichosheheni abiria 50 kutoka eneo la Narayanganj katikati mwa nchi kuongana na meli ya mizigo. Mnamo mwezi Juni mwaka jana, kivuko kilizama huko Dhaka baada ya kugongwa nyuma na feri nyingine. Angalau watu 32 walifariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.