Pata taarifa kuu
BANGLADESHI-USALAMA

Bangladesh: Siku ya tatu ya makabiliano makali ya kidini kati ya Wahindu na Waislamu

Kwa siku ya tatu mfululizo, Bangladesh inakumbwa na mivutano ya kidini kati ya Waislam walio wengi na Wahindu walio wachache, makabiliano ambayo yamesababisha vifo vya watu 4 na wengine 150 wamejeruhiwa.

Waandamanaji wanakimbia baada ya kuwatupia mawe maafisa wa polisi wakati wa maandamano karibu na msikiti huko Dhaka Oktoba 15, 2021, siku ya tatu ya vurugu za kidini.
Waandamanaji wanakimbia baada ya kuwatupia mawe maafisa wa polisi wakati wa maandamano karibu na msikiti huko Dhaka Oktoba 15, 2021, siku ya tatu ya vurugu za kidini. © Munir Uz zaman, AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya vitendo vya uharibifu wa maeneo ya ibada ambavyo vilibadilika kuwa mapigano huko Dhaka na Chittagong, hasa, maelfu ya waumini wameandamana Ijumaa (Oktoba 15) katika mji mkuu dhidi ya kile wanachokiona kama tusi kwa Uislamu.

Chanzo cha vurugu hiyo ni video ambayo imesamba kwenye mitandao ya kijamii. Inaonyesha nakala za kitabu kitukufu kwa Waislamu, Quran, zikiwekwa chini ya mguu wa mungu wa Wahindu.

Siku ya Jumatano Oktoba 13, wakati Wahindu walisherehekea Durga Puja, sikukuu yao kubwa ya kidini huko Bangladesh, umati wa watu wasiopungua 500 walivamia kanisa ya Wahindu huko Hajiganj. Kutokana na tukio hilo, polisi waliwafyatulia risasi umati wa watu, na kusababisha vifo vya watu wanne.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mapigano makali ya kidini yaliyoambatana na mfululizo wa uharibifu na vitendo vya uharibifu dhidi ya maeneo ya ibada ya Wahindu. Kwa jumla, mahekalu 80 yalishambuliwa au kuteketezwa kwa siku tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.