Pata taarifa kuu

Amnesty International yatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kutoa msaada Syria

Nairobi – Shirika la  kutetea haki za binaadamu la Amnesty Internationale latoa wito kwa umoja wa Mataifa kuendelea kutoa misaada kwa wahasiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Syria .Nchi hiyo ilikumbwa na tetemeko la ardhi kupitia vivuko viwili katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi .


Malori yakiwa yamepakia misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria kufuatia tetemeko kubwa la ardhi.
Malori yakiwa yamepakia misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria kufuatia tetemeko kubwa la ardhi. AP - Ghaith Alsayed
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Februari 6, tetemeko kubwa la ardhi lilishuhudiwa Uturuki na Syria, na kuua zaidi ya watu  elfu 55,000 katika nchi zote mbili.

Mkuu  wa Umoja wa Mataifa alisema mnamo Februari 13 kwamba Rais wa Syria Bashar al-Assad alikubali kufungua vivuko vya Bab al-Salama na Al-Rai kutoka Uturuki ili kuruhusu msaada kuingia kwa kipindi cha awali cha miezi mitatu.

Umoja wa Mataifa "lazima uendelee kutoa msaada" kupitia njia hizo mbili baada ya Mei 13 "bila kujali kama serikali itaongeza" ridhaa yake, Amnesty ilisema katika taarifa.

Kabla ya maafa, karibu misaada yote muhimu ya kibinadamu kwa zaidi ya watu milioni nne wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi kaskazini na kaskazini magharibi mwa Syria ilikuwa ikitolewa kutoka Uturuki kupitia mfereji mmoja kivuko cha Bab al-Hawa.

Idadi ya vivuko vilivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kuingia Syria ilipungua kutoka nne mwaka 2014, baada ya miaka mingi ya shinikizo kutoka kwa washirika wa serikali China na Urusi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Siku tatu baada ya tetemeko hilo, msafara wa kwanza wa misaada ya Umoja wa Mataifa ulivuka kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Syria na kubeba mahema na vifaa vingine ambavyo vilitarajiwa kabla ya maafa hayo, na hivyo kuzua shutuma kali kutoka kwa makundi ya kibinadamu na wanaharakati wa eneo hilo.

"Maisha ya zaidi ya watu milioni nne yako hatarini na sheria za kimataifa ziko wazi kwamba haki zao lazima ziwe kuu," Sherine Tadros wa Amnesty alisema katika taarifa hiyo.

   "Umoja wa Mataifa unapaswa kuchukua msimamo wazi dhidi ya njama za kikatili za kisiasa ambazo zimetatiza operesheni zake za kibinadamu kaskazini mwa Syria kwa miaka kadhaa," Tadros aliongeza.

Waasi wanaoungwa mkono na Uturuki wanaendesha vivuko vya Bab al-Salama na Al-Rai katika jimbo la kaskazini la Aleppo, huku kundi la wanajihadi la Hayat Tahrir al-Sham likidhibiti Bab al-Hawa katika eneo la Idlib.

Umoja wa Mataifa ulikadiria mapema wiki hii kwamba Syria inahitaji karibu dola bilioni 15 ili kupata nafuu kufuatia tetemeko hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.