Pata taarifa kuu

Washington: Marekani na India zamaliza mzozo wa hivi punde wa kibiashara

Washington imetangaza siku ya Ijumaa Septemba 8, 2023 kwamba imefikia makubaliano na New Delhi kutatua mzozo wa hivi karibuni wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, wakati Joe Biden, nchini India kwa ajili ya mkutano wa G20, amekutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Joe Biden na Narendra Modi wakati wa chakula cha jioni cha serikali katika Ikulu ya White mnamo Juni 22, 2023.
Joe Biden na Narendra Modi wakati wa chakula cha jioni cha serikali katika Ikulu ya White mnamo Juni 22, 2023. AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu "ni hatua muhimu katika uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na India," amesema mwakilishi wa White House anayehusika na biashara, Katherine Tai, aliyenukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari. Matangazo haya, aliongeza, "yanasisitiza nguvu ya ushirikiano wetu wa nchi mbili."

Hayo yanajiri wakati kongamano la mataifa tajiri na yenye uwezo kiuchumi litaanza rasmi kesho Jijini New Delhi nchini India.Kufikia sasa baadhi ya viongozi wameelekea huko akiwemo rais wa marekani Joe Biden wakati huu kukiwa na taarifa kuwa kunao viongozi ambao hawatahudhuria.

Rais wa Marekani Joe Biden anatumai kutumia nafasi ya kukosekana kwa viongozi hao wawili , Xi Jinping  na Putin ili kuimarisha ushawishi wa Washington.

Viongozi hao wanakutana wakati huu kukiwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia  vita vya Ukraine na jinsi ya kuyasaidia mataifa yanayoinukia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.Juzi tuu marekani iliipa msaada wa ndege zisizo na rubani nchi ya Ukraine.Swala ambalo urusi ilisema nikinyume na ubinaadamu.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesisitiza dhamira ya kutanua kundi hilo kwa kujumuisha Umoja wa Afrika kama mwanachama wa kudumu.

Mwaka jana viongozi hao walikutana kwa mkutano wa kilele huko Bali, Indonesia, ili kuleta afueni kwa uchumi unaokumbwa na mgogoro na angalau kuwapatanisha Urusi na Ukraine.

Katika miaka ya hivi karibuni, bara la Afrika limealikwa kwa utaratibu kwenye mikutano ya kilele ya kundi hili. Mwaka huu, uwepo wake ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwa kuzingatia majanga mengi yanayoathiri Afrika, iwe uhaba wa chakula, hali ya hewa, nishati au madeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.