Pata taarifa kuu

India: Shule zafungwa New Delhi kutokana na kukosa hewa katika wingu la uchafuzi wa mazingira

Nchini India, viongozi katika mji mkuu wameamuru kufungwa kwa shule za msingi Ijumaa hii asubuhi na vile vile vizuizi vya usafiri ili kukabiliana na wimbi kubwa la uchafuzi wa hewa. New Delhi imefunikwa na wingu zito la sumu kwa zaidi ya wiki moja, na inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika siku zijazo.

Ukungu wa uchafuzi wa mazingira katika mji mkuu wa India, New Delhi, Novemba 3, 2023.
Ukungu wa uchafuzi wa mazingira katika mji mkuu wa India, New Delhi, Novemba 3, 2023. AP - Shonal Ganguly
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko New Delhi, Sébastien Farcis

Tahadhari hiyo ilitolewa Alhamisi jioni, wakati kiwango cha chembechembe laini katika hewa ya New Delhi kilizidi maikroni 400 kwa kila mita ya ujazo, au mara 26 ya viwango vilivyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani kwa zaidi ya saa 24. Sababu moja ni kuongezeka maradufu kwa idadi ya mioto ya kilimo katika maeneo jirani, iliyoanzishwa na wakulima ili kuondoa makapi yao.

Zaidi ya matukio 2,000 ya moto yaliripotiwa wakati wa mchana. Moshi wao sasa unachangia robo ya uchafuzi wa mazingira, na iliyobaki ikitoka kwa moshi wa magari au mitambo ya kuzalisha nishati ya makaa ya mawe katika eneo hilo. Watoto, ambao mapafu yao bado yanaendelea kukuwa, wako katika hatari. Na kwa hivyo shule za msingi zimefungwa siku ya Ijumaa, Novemba 3, wanafunzi wanafuata visomo vyao mtandaoni, hali ambayo ni changamoto kwa familia zenye kipato cha chini.

Maeneo ya ujenzi yasiyo ya lazima pia yameingiliwa ili kuepuka kutawanyika kwa vumbi, na magari ya zamani yamepigwa marufuku kutembea. Hewa hii ya chafu inapaswa kuendelea, au hata kuwa mbaya zaidi, katika muda wa wiki mbili zijazo, na kuongezeka kwa mioto na sherehe ya Diwali, tamasha la mwanga (taa).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.