Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Matetemeko ya ardhi Japani: Marekani iko tayari kutoa 'msaada wowote muhimu'

Rais wa Marekani Joen Biden amehakikisha siku ya Jumatatu usiku, Januari 1 kwamba Marekani iko tayari kutoa "msaada wowote muhimu" kwa Japan baada ya matetemeko makubwa ya ardhi ambayo yalipiga nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu sita.

Nyufa ardhini huko Wajima, Mkoa wa Ishikawa, Japani, Jumatatu, Januari 1, 2024, kufuatia tetemeko la ardhi.
Nyufa ardhini huko Wajima, Mkoa wa Ishikawa, Japani, Jumatatu, Januari 1, 2024, kufuatia tetemeko la ardhi. AP
Matangazo ya kibiashara

"Utawala wangu unawasiliana na maafisa wa Japan na Marekani iko tayari kutoa msaada wowote muhimu kwa raia wa Japan," amesema katika taarifa, akikumbusha kuwa Japan na Marekani "ni washirika wa karibu.

Matetemeko makubwa ya ardhi yamepiga katikati mwa Japani siku ya Jumatatu usiku, na kusababisha uharibifu mkubwa na kusababisha pia tsunami yenye urefu wa zaidi ya mita moja katika maeneo, huku watu katika maeneo yaliyoathiriwa wakitakiwa kuhama hadi sehemu za juu.

Mapema siku ya Jumanne, mamlaka ya Japani imethibitisha vifo vya watu wanne baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.5 kupiga Mkoa wa Ishikawa, upande wa Bahari ya Japan ya kisiwa kikuu cha Honshu, saa 1O:10 alaasiri kwa saa za Japana, kulingana na Taasisi ya Marekani ya Jiofizikia (USGS).

Zaidi ya matetemeko 50 ya ardhi ndani ya masaa machache tu

Vituo vya televisheni vilikatiza matangazo yao ya kawaida kwa kutangaza vipindi maalum. Wakati huo huo Waziri Mkuu Fumio Kishida amewataka wakazi katika maeneo hatari "kuhama haraka iwezekanavyo" hadi maeneo ya juu.

Waziri wa Ulinzi Minoru Kihara almeangaza kuwa wanajeshi 1,000 wanajiandaa kwenda katika eneo hilo, huku wengine 8,500 pia wakiwa wako tayari kutumwa katika eneo la tukio. Karibu ndege ishirini za kijeshi zilitumwa kutathmini uharibifu.

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japani (JMA) imerekodi zaidi ya matetemeko 50 ya ukubwa wa 3.2 au zaidi katika muda wa saa nne kwenye Rasi ya Noto, kaskazini mwa Wilaya ya Ishikawa, inayopakana na Bahari ya Japani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.