Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Bangladesh inawachagua wabunge, uchaguzi uliosusiwa na upinzani

Raia wa Bangladesh milioni mia moja na ishirini wanapiga kura Jumapili hii, Januari 7, kwa uchaguzi wa wabunge uliohakikishiwa kumpa Waziri Mkuu Sheikh Hasina muhula wa nne mfululizo, baada ya kususia vyama vya upinzani.

Bango la uchaguzi unaotoa nafasi kubwa ya kushinda kwa Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina mnamo Januari 3, 2024 huko Dhaka.
Bango la uchaguzi unaotoa nafasi kubwa ya kushinda kwa Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina mnamo Januari 3, 2024 huko Dhaka. © Mohammad Ponir Hossain / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hizi ni chaguzi ambazo matokeo yake yanaonekana tayari yameandikwa. Kutokana na kukosekana kwa chama kikuu cha upinzani, Bangladesh Nationalist Party (BNP), ambacho kiliamua kususia zoezi la upigaji kura, Waziri Mkuu Sheikh Hasina, aliye madarakani bila kukatizwa tangu 2009, anahakikishiwa kushinda kwa muhula wa nne mfululizo. "Kushiriki uchaguzi chini ya Bi. Hasina, kinyume na matarajio ya watu wa Bangladesh, kutadhoofisha dhabihu za wale waliopigana, kumwaga damu na kutoa maisha yao kwa ajili ya demokrasia," amesema kiongozi wa BNP aliye uhamishoni Tarique Rahman.

Chama kikuu cha upinzani kinazingatia kwamba serikali, ambayo inadhibiti utawala mzima, itahuska na wizi wa kura. "Inaanza wakati wa uteuzi," anaelezea Shahdeen Malik, msimamizi wa Kituo cha Majadiliano ya Sera, akihojiwa na mwandishi wetu wa kikanda, Sébastien Farcis. Kuna mtihani wa kuingia katika utawala, na mara wagombea watakubaliwa, polisi lazima idhinishe wasifu wao. Hii ni kawaida ili kuhakikisha kwamba hawana historia ya uhalifu, lakini nimeona kesi nyingi ambapo walikataliwa kuingia katika utawala kwa sababu ya utii wao wa kisiasa au wa familia zao. Na hii inatia siasa kwenye utawala. Hili ni muhimu zaidi kwa muonekano, ambao sasa unategemea tu masuala ya kisiasa. "

Kutokana na kususia huko, chama cha Sheikh Hasina, Amawi League, hakina wapinzani kivitendo katika majimbo wanakogombea. Lakini alishindwa kusimamisha wagombea katika wachache wao, kwa nia ya dhahiri ya kuzuia Bunge la umoja huo kuonekana kama chombo cha chama kimoja. Baadhi ya wapiga kura wanasema walitishiwa kunyang'anywa kadi zao za manufaa za serikali, muhimu ili kupata manufaa ya kijamii, ikiwa watakataa kupigia kura chama cha Awami League.

Ukandamizaji

Chama kikuu cha upinzani cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) na vyama vingine vilifanya maandamano mwaka jana kumtaka waziri mkuu kujiuzulu na kuendeleza serikali ya mpito isiyoegemea upande wowote kusimamia uchaguzi huo, bila mafanikio. Baadhi ya makada 25,000 wa upinzani, wakiwemo viongozi wote wa ndani wa BNP, walikamatwa katika wimbi la ukandamizaji lililofuata, kwa mujibu wa chama hicho. Serikali, kwa upande wake, iliripoti kukamatwa  kwa watu 11,000.

Jumamosi hii asubuhi, tena, afisa mkuu wa BNP na wanaharakati sita walikamatwa huko Dhaka, mji mkuu. Wanatuhumiwa kwa hujuma baada ya moto katika treni ya abiria na kusababisha vifo vya takriban watu wanne siku ya Ijumaa. Visa kadhaa vya moto vimetokea tangu mwaka jana kwenye mtandao wa reli, unaoelezewa kama "vitendo vibaya vya hujuma" na polisi, ambao wanashutumu BNP kwa kuhusika na shambulio hilo. Chama cha upinzani kwa upande wake kinakanusha kuhusika kwa namna yoyote, na kwa upande wake kinashutumu mamlaka kwa kuchochea moto huu ili kuweza kuwashutumu wapinzani na kuongoza kampeni ya ukandamizaji dhidi yake.

Mandhari ya kisiasa katika nchi hiyo yenye watu milioni 170 kwa muda mrefu yametawaliwa na uhasama kati ya Sheikh Hasina, bintiye mwanzilishi wa nchi hiyo, na Khaleda Zia, waziri mkuu mara mbili na mke wa kiongozi wa zamani wa kijeshi. Sheikh Hasina, 76, ametawala tangu arejee madarakani mwaka 2009, na kuimarisha udhibiti wake baada ya chaguzi mbili zilizokumbwa na kasoro na shutuma za udanganyifu.

Uchumi uliodorora

Wakati serikali ya Bangladesh inashutumiwa mara kwa mara kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa kikatili wa upinzani, mafanikio ya sera yake ya kiuchumi kwa muda mrefu yamehakikisha umaarufu wa Waziri Mkuu wake. Kwa hakika Bangladesh ni mojawapo ya nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi duniani, ikiwa na kiwango cha karibu 7% kwa mwaka, ikisukumwa na sekta ya nguo, ambayo inazalisha 85% ya dola bilioni 55 katika mauzo ya nje ya kila mwaka kutoka nchini humo. Serikali imehitimisha miradi mingi ya miundombinu ili kuboresha usafirishaji wa bidhaa, kama vile Daraja kubwa la Padma. Lakini mzozo wa Uviko na kupanda kwa bei ya mafuta tangu vita vya Ukraine kumesababisha mfumuko wa bei kupanda hadi zaidi ya 10% kwa mwaka, na kuongeza nakisi ya umma.

Lakini matatizo yameongezeka hivi karibuni, na kupanda kwa bei ya bidhaa za msingi na kuenea kwa umeme kukatika katika mwaka 2022. Kutokana na mfumuko huu wa bei, maelfu ya wafanyakazi wa nguo wameongoza harakati za kihistoria za mgomo, unaochochewa na moto katika viwanda kadhaa na kukandamizwa vikali kwa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.