Pata taarifa kuu

Bangladesh: Uchaguzi wasusiwa kwa kiwango kikubwa, Sheikh Hasina apewa nafasi ya kushinda

Vituo vya kupigia kura vimefungwa nchini Bangladesh katika uchaguzi wa wabunge bila mashaka yoyote ya kweli: chama kikuu cha upinzani, cha BNP, kimesusia uchaguzi wakipinga tume ya uchaguzi kuwa na upendeleo. Waziri Mkuu Sheikh Hasina, aliye madarakani kwa miaka kumi na mitano, kwa hivyo anahakikishiwa kushinda kwa muhula wa nne mfululizo. Suala pekee katika uchaguzi huu lilikuwa ni ushiriki, lakini hili ni jambo la kukatisha tamaa.

Waziri Mkuu, Sheikh Hasina (picha yetu ya kielelezo), aliye madarakani kwa miaka kumi na tano, ana uhakika wa kushinda kwa awamu ya nne mfululizo.
Waziri Mkuu, Sheikh Hasina (picha yetu ya kielelezo), aliye madarakani kwa miaka kumi na tano, ana uhakika wa kushinda kwa awamu ya nne mfululizo. AFP PHOTO/POOL/OLI SCARFF
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kanda, Sébastien Farcis

Ushiriki katika cuchaguzi huu wa wabunge ulikuwa karibu 40%, kulingana na Tume ya Uchaguzi. Kwa hivyo zaidi ya nusu ya wapiga kura wa Bangladesh wamesusia uchaguzi huu bila changamoto yoyote, kutopiga kura mara mbili ya miaka mitano iliyopita.

Kinyume

Hii inaenda kinyume na dau la chama tawala cha Awami League, ambacho kilitaka kukabiliana na kususia kwa upinzani kwa kuonyesha kwamba bado kulikuwa na changamoto fulani, na kwa hivyo ushiriki mkubwa. Dau ambalo halikufaulu.

Matukio

Matukio kadhaa yamegubika siku hii ya kupiga kura: bomu lilirushwa karibu na kituo kimoja cha kupigia kura huko Dhaka, na kuwajeruhi watu wanne. Mgombea kutoka chama tawala cha Awami League alienguliwa baada ya kutishia maafisa wa polisi, na wagombea huru wanane walijiunga na wagombea wangine kususia kura baada ya waangalizi wao kudaiwa kufukuzwa kwenye vituo vya kupigia kura na wafuasi wa Awami wakidaiwa kujaza masanduku ya kupigia kura, masanduku ya kura yaliyokuwa yamejazwa awali. Uchunguzi umeanzishwa kuhusu suala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.