Pata taarifa kuu

Burma: utawala wa kijeshi unashutumu UN kwa 'madai ya upendeleo' kuhusu haki za binadamu

Serikali ya kijeshi iliyoko madarakani nchini Burma imeshutumu "madai ya upendeleo" ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na kutangaza kwamba haikuwa imefahamishwa rasmi kuhusu kuteuliwa kwa mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa Myanmar wanashiriki gwaride la kuadhimisha Siku ya 78 ya Wanajeshi wa nchi hiyo huko Naypyidaw mnamo 2023 (picha ya kielelezo).
Wanajeshi wa Myanmar wanashiriki gwaride la kuadhimisha Siku ya 78 ya Wanajeshi wa nchi hiyo huko Naypyidaw mnamo 2023 (picha ya kielelezo). AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi ya Kusini-mashariki mwa Asia ya Burma vimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni na vikosi vinavyopinga jeshi - ambalo lilichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021, na kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia - vimeendelea kote nchini. Wiki iliyopita, Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kulaani "ukiukwaji wa kutisha wa haki za binadamu" nchini Burma. Umoja wa Mataifa pia umekosoa "kushikilia" kwa serikali ya kijeshi juu ya misaada ya kibinadamu, ambayo inazidisha mzozo ambao umesababisha zaidi ya watu milioni 2.5 kuyahama makazi yao.

"Tuhuma zisizo na msingi na zenye upendeleo"

Azimio ambalo "lina madai yasiyo na msingi na ya upendeleo," wizara ya mambo ya nje ya utawala wa kijeshi w burma imesema katika taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la serikali la Global New Light la Myanmar. "Kwa hivyo, Burma inakataa kabisa azimio hilo." Kwa mujibu wa taarifa hii kwa vyombo vya habari, "hakuna mtaarifa rasmi iliyotolewa kwa Burma" kuhusu uteuzi, wiki iliyopita, wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alimteua Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Australia Julie Bishop katika wadhifa uliokuwa wazi tangu kuondoka kwa mtangulizi wake mwezi Juni 2023. Noeleen Heyzer raia wa Singapore alitembelea Burma mwaka 2022 na kukutana na kiongozi wa utawala wa kijeshi Min Aung Hlaing, hatua ambayo ilikosolewa na makundi ya haki za binadamu. Lakini alikataliwa kukutana na Aung San Suu Kyi, kiongozi mkuu wa demokrasia ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka ishirini na saba jela kilichotolewa na mahakama ya kijeshi iliyokutana kwa fadragha.

Kisha aliwakasirisha maafisa wa serikali ambao walimshtumu kwa kutoa "taarifa ya upande mmoja" ya kile kilichojadiliwa. Balozi wa Burma (Myanmar) katika Umoja wa Mataifa, Kyaw Moe Tun, aliteuliwa na serikali ya kiraia ya Suu Kyi na alikataa kuondoka wadhifa wake licha ya msisitizo wa serikali ya kijeshi tangu kuchukua madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.