Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: wanawake waandamana dhidi ya marekebisho ya Katiba

Alhamisi Oktoba 30, wabunge wa Burkina Faso wataamua kupitisha au la muswada wa sheria uliyoandaliwa na serikali kwa ajili ya marekebisho ya Katiba.

Katika mitaa ya mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, Oktoba 27 mwaka 2014.
Katika mitaa ya mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, Oktoba 27 mwaka 2014. Photo RFI / Yaya Boudani
Matangazo ya kibiashara

Iwapo muswada huo wa sheria utapitishwa, rais Blaise Compaoré atakua amepewa nafasi ya kugombea kwa muhula mwengine katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwaka 2015.

Upinzani umetolea wito raia kuandamana Jumanne Oktoba 28 ili kupinga uamzi wa serikali ya kuifanyia marekebisho Katiba. Lakini tangu Jumatatu Oktoba 27, wanawake wameingia mitaani kuonyesha hasira zao dhidi ya marekebisho hayo ya Katiba.

 Jumatatu Oktoba 27, mamia ya wanawake kutoka vyama vya siasa na mashirika ya kiraia waliingia mitaani na kuandamana wakipinga marekebisho ya Ibara ya 37 ya Katiba ya Burkina Faso, ambayo hamruhusu rais Blaise Compaoré kugombea kwa muhula mwengine. Wanawake hao wameandamana wakiwa na miko mikononi, huku wakiimba nyimbo zinayoikashifu serikali. Wanawake hao wameiomba serilkali kuondoa Bungeni muswada huo wa sheria.

“ Tumejitokeza mitaani tukiwa na miko ili kumuonya mtu huyo ambaye lengo lake ni kuliweka hatarini taifa la Burkina Faso”, ameeleza Juliette Congo naibu kiongozi wa chama cha upinzani MPP, akibaini kwamba kura ya maoni na marekebisho ya Katiba vitasababisha Burkina Faso inaingia katika dimbwi la machafuko.

“ Tumeamua kumwambia rais Compaoré kwamba tunamheshimu kama rais, lakini hatukubaliane naye. Na miko hii ni onyo kwake. Iwapo Blaise Compaoré hatobadilisha uamzi wake kuanzia usiku wa Jumanne Oktoba 28, wanawake wa Burkina Faso watakua kwenye mstari wa mbele kwa kuandamana wakipinga uwezekano wowote wa kuifayia marekebisho Katiba”, ameongeza Juliette Congo.

Idadi kubwa ya askari polisi iliyowekwa mitaani ili kuzuia maandamano hayo haikukataza wanawake hao kuandamana wakianzia katika jengo la Bunge hadi makao makuu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mjini Ouagadougou.

Hayo yanajiri wakati ambapo vyama vya upinzani nchini Burkina Fasso vimeandaa maandamano makubwa Jumanne Oktoba 28 kupinga marekebisho ya katiba ambayo yanatafsiriwa na wanasiasa wa nchi hiyo na wadau wengine kuwa ni mbinu ya kumruhusu rais Blaise Compaore kuendelea kubaki madarakani.

Ibara ya 37 ya Katiba ya Burkina Fasso hamruhusu rais kugombea baada ya mihula miwili kama ilivyo sasa kwa rais Blaise Compaore na ambapo siku ya Alhamisi wabunge wa nchi hiyo wanatarajiwa kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.