Pata taarifa kuu
SYRIA-IRAQ-UTURUKI-ISIL-KOBANE-Usalama

Syria: Wapeshmerga wa Iraq wawasili pembezuni mwa Kobane

Wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq wamewasili usiku wa kuamkia Jumatano Okoba 29 pembezuni mwa mji wa Kobane, bila hata hivo kuingia katika mji huo.

Msafara wa wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq (peshmerga) wakipitia Erbil (mji mkuu wa Kurdistann chini Iraq) ili waweze kuingia Kobane, Oktoba 28, 2014.
Msafara wa wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq (peshmerga) wakipitia Erbil (mji mkuu wa Kurdistann chini Iraq) ili waweze kuingia Kobane, Oktoba 28, 2014. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Mji huo ulioko kaskazini mwa Syria kwenye mpaka wa Uturuki umezingirwa kwa majuma kadhaa na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kuwasili kwao kulikuwa kukisubiriwa, wiki moja baada ya Uturuki kuruhusu wapiganaji hao kutumia ardhi yake kwa kuingie katika mji wa Kobane.

Wapiganaji hao wa Kikurdi wa Iraq waliwasili Uturuki usiku, baada ya kuondoka Kurdistan Jumanne mchana Oktoba 28 wakijielekeza kusaidia ili mji wa Kobane usianguki mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Mji huo wa Kobane umezingirwa kwa majuma kadhaa na wapiganaji wa Dola la Kiislam. Serikali ya Ankara ilitangaza hivi karibuni kwamba inawaruhusu wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq kutumia ardhi yake kwa kuingia katika mji wa Kobane. Wapiganji hao wa Kikurdi ni 150, ambao wako katika makundi mawili.

Kundi la kwanza linaloundwa na wapiganaji 76, limewasili saa tisa na nusu usiku saa za Uturuki kwenye uwanja wa Sanliurfa kwenye umbali wa kilomita 50 na mpaka wa Uturuki na mji wa Kobane. Wapiganji hao walisafirishwa na ndege ya Uturuki, Turkish Airlines. Walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Sanliurfa, wapiganaji hao walisafirishwa kwa mabasi yakishindikizwa na vifaru vya jeshi la Uturuki hadi katika eneo la Mursitpinar, ambako wanasubiri kuingia katika mji wa Kobane

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.