Pata taarifa kuu
MAREKANI-BURKINA FASO-Maandamano-Siasa

Washington yatiwa wasiwasi na hali inayojiri Burkina Faso

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya Marerkani, Jumanne jioni Oktoba 28, Washington inatiwa wasiwasi si tu kwa maandamano yaliyoibuka hivi karibuni nchini Burkina Faso, lakini pia mchakato wa marekebisho ya Katiba ambayo serikali imeanzisha.

waandamanaji wakipinga marekebisho ya Katiba, kwenye eneo la taifa, Ouagadougou, Jumanne Oktoba 28 mwaka 2014.
waandamanaji wakipinga marekebisho ya Katiba, kwenye eneo la taifa, Ouagadougou, Jumanne Oktoba 28 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo wa sheria utawasilishwa bungeni Jumatano Oktoba 29.

Kuhusu mchakato wa Katiba ambao unaendelea nchini Burkina Faso, tangazo la msemaji wa waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry ameelezea "wasiwasi wake kuhusu nia ya serikali ya Burkina Faso ya kujaribu kuunda muswada wa sheria wenye lengo la kuifanyia marekebisho Katiba ili kumpa nafasi rais Blaise Compaore Kugombea kwa muhula mwengine wa miaka mitano". Rais Blaise Compaoré haikutajwa.

Taarifa hiyo inaenda sambamba na msimamo wa Barack Obama wakati wa mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika mwezi Agosti mwaka 2014. Rais Barack Obama, aliwaambia marais wa mataifa ya Afrika waliyokua walishiriki mkutano huo kwamba, Marekani haitounga mkono rais yeyote atakaye jaribu kusalia madarakani, hata kama atakua ameleta maaendeleo katika nyanja mbalimba za nchi yake, aidha utendaji wake wa kazi, na kudumisha amani.

Tangazo hilo la wizara ya mambo ya nje ya Marekani limeeleza kwamba "mipaka ya kikatiba, na uchaguzi ni taratibu zisiyo badilishwa kwa lengo kukabidhiana madaraka katika misingi ya kidemokrasia na amani bila vurugu zozote, ili kukipa nafasi kizazi kipya kwa uongozi wa nchi". Katika tangazo hilo, msemaji wa John Kerry amevitaka vikosi vya usalama vya Burkina Faso kuendelea kazi yao bila vurugu, wakati ambapo hali ya wasiwasi imetanda nchi nzima.

Siku ya Jumanne, maandamano makubwa yameshuhudiwa kufanyika nchi nzima na hasa katika mji mkuu wa Ouagadougou ambapo watu wapatao milioni moja wanaripotiwa kushiriki kupinga marekebisho ya Katiba ya nchi hiyo, jambo ambalo linazungumziwa na waandaaji kama mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.