Pata taarifa kuu

Polisi ya Kenya yachunguza kifo cha wakili aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya ICC

Mamlaka nchini Kenya imefungua uchunguzi kuhusu kifo cha wakili anayedaiwa kuwahonga na kuwatisha mashahidi wakati wa mashtaka ya Rais William Ruto katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), afisa wa polisi amesema Jumanne.

Wakili Paul Gicheru katika mahakama ya ICC mnamo Februari 2022.
Wakili Paul Gicheru katika mahakama ya ICC mnamo Februari 2022. © CPI
Matangazo ya kibiashara

Paul Gicheru alishutumiwa na waendesha mashtaka wa ICC kwa kuanzisha mfumo "dhahiri na mbaya" wa kuvuruga mashahidi na hivyo kushindwa kuendelea na uchunguzi dhidi ya Bw Ruto kwa madai ya kuhusika katika ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka wa 2007 na 2008.

Wakili huyo, mwenye umri wa miaka 50, alipatikana amekufa usingizini Jumatatu jioni katika makazi yake huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Kesi ya Bw. Gicheru ilianza mwezi Februari mjini Hague. Waendesha mashtaka walisema wakili huyo aliwahonga mashahidi kwa kuwalipa hadi shilingi milioni moja za Kenya (takriban euro 8,300) na kuwatishia wengine, akiwemo mmoja kwa bunduki.

Bw. Gicheru alikuwa amekanusha mashtaka hayo, huku akikana mashtaka mbele ya mahakama ya ICC, iliyoko Hague.

"Taarifa tulizonazo kutoka kwa familia yake ni kwamba alikula chakula kisha akaenda kulala lakini hakuamka," afisa wa polisi ambaye aliomba kutotajwa jina lake ameliambia shirika la habari la AFP.

“Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo chake,” afisa huyo amesema na kuongeza kuwa mwanawe Bw Gicheru alipelekwa hospitalini baada ya kulalamikia maumivu ya tumbo baada ya kuchangia chakula.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya kwenye Twitter imezitaka mamlaka "kufanya uchunguzi wa haraka na wa mwisho" kuhusu chanzo cha kifo, huku ikisema "imesikitishwa na habari hii ya kushtua".

Ghasia za baada ya uchaguzi wa mwishoni mwa 2007- mapema 2008 zilisababisha vifo vya zaidi ya 1,300 na 600,000 kuhama makwao nchini Kenya baada ya uchaguzi wa 2007.

Mnamo 2014, ICC iliondoa mashtaka dhidi ya Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu kwa madai ya kuhusika katika ghasia hizo.

Kisha, Aprili 2016, alitupilia mbali kesi hiyo kwa manufaa ya Makamu wa Rais William Ruto na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang, kushtakiwa katika kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.