Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Uganda: Mahakama ya Kikatiba yatathmini sheria yenye utata

Serikali kwa upande wake imetetea sheria hiyo ikisema inalenga kusaidia makundi ya haki na mashirika yanayotoa misaada. imesema imefanya maboresho katika ulinzi wa haki za binadamu katika miaka ya hivi karibuni.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni mnamo Januari 16, 2022, katika makazi yake huko Kisozi.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni mnamo Januari 16, 2022, katika makazi yake huko Kisozi. REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Katiba ya Uganda siku ya Ijumaa ilisikiliza hoja kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yakikosoa sheria ya mwaka 2016 ambayo wanasema inaipa serikali mamlaka ambayo haijawahi kushuhudiwa kudhibiti mashirika ya kiraia, huku serikali badala yake ikisema inasaidia kuilinda vyema.

Kwa upande wa mashirika ya Chapter Four Uganda na Center for Constitutional Governance yanasema sheria inaweka mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye 'udhibiti mkubwa wa serikali na kuingiliwa katika masuala yao kwa upana na serikali' itaathiri haki ya kuwa na uhuru wa kujieleza na kujumuika zinazohakikishwa kikatiba nchini Uganda.

Baadhi ya Ibara za sheria zinawezesha serikali kufungia shirika kwa sababu ambazo "ni za jumla sana na zisizoeleweka", wamesema. Zinasababisha uwezekano wa "taratibu za kiutawala zenye vikwazo na ngumu" na vikwazo vya uhalifu dhidi ya mashirika ya kiraia, ame Anthony Masake, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Chapter Four Uganda..

"Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita," utekelezaji wa sheria umekuwa na "madhara makubwa juu ya uwezo wa raia kutumia haki zao kwa uhuru," ameliambia shirika la habari la AFP. Hakuna tarehe ya mwisho iliyowekwa kwa uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba katika kesi hii.

Mwanzoni mwa mwezi Februari, serikali ilitangaza kwamba haitarejea upya mamlaka ya ofisi ya ndani ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, ambayo inaisha mwishoni mwa mwaka, ikizingatiwa kuwa "imetengeneza taasisi za ndani zenye nguvu za kutosha juu ya 'haki za binadamu'.

Uamuzi huu ulikosolewa na Muwada Nkunyingi, mwanachama wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa linaloongozwa na Robert Kyagulanyi, almaarufu Bobi Wine, mmoja wa wapinzani wakuu wa Rais Yoweri Museveni ambaye ametawala Uganda kwa mkono wa chuma tangu 1986. Anasema, 'serikali inataka kukiuka haki za binadamu bila vikwazo.'

Wakati wa uchaguzi uliopita wa urais, mwaka wa 2021, waandishi wa habari walishambuliwa, mawakili kufungwa na viongozi kadhaa wa upinzani kunyamanzishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.