Pata taarifa kuu

Mratibu wa EAC: Amani imeanza kurejea mashariki ya DRC

NAIROBI – Hatua Mratibu wa mazungumzo ya amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Kenya, anasema hatua imeanza kupigwa, kurejesha amani na utulivu katika mikoa ya Mashariki mwa DRC.

Rais wa zamani wa Kenya ambaye ndiye mratibu wa EAC nhini DRC
Rais wa zamani wa Kenya ambaye ndiye mratibu wa EAC nhini DRC © Monicah Mwangi / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta, kupitia kwa taarifa yake amesema baada ya mikutano mitatu ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya usalama Mashariki mwa DRC, hali ya utulivu inashuhudiwa jimboni Kivu Kusini, lakini pia visa vya mashambulio vimepungua huko Kivu Kaskazini ila hali bado ni ya kutia wasiwasi.

Hata hivyo, amesema juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu waliothiriwa na utovu wa usalama, zinaendelea vema, na jeshi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, limeanza kuchukua miji na vijiji vilivyokuwa vinashikiliwa na makundi ya waasi.

Aidha, mratibu huyo amedokeza kuwa, mipango inaendelea ili kuandaa mkutano wa wadau wote wa mzozo huu pamoja na watalaam kutoka nje ya nchi, kuthathmini namna ya kupata suluhu ya kisiasa, mazunngumzo yatakayofanyika Mashariki mwa DRC.

Kuhusu kuondoka kwa waasi wa M 23 katika maeneo wanayoshikilia,mratibu huyo amedokeza kuwa kundi hilo litaondoka katola maeneeo ya Sake, Mshaki, Neero na Kilolirwe  kuanzia siku ya Jumanne wiki hii, na hii inakuja baada ya kuwasili kwa wanajesjhi wa Sudan Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kikosi cha Kenya kipo katika eneo la Kibati, Kibumba na Rumangambo, kile cha Burundi kikiwa katika eneo la Sake, Mshaki na kinatarajiwa kwenda Kitchanga na kile cha Uganda ambacho kipo Bunagana kinatarajiwa kudhibiti Kiwanja ifikikapo Aprili 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.