Pata taarifa kuu

DRC: Zaidi ya raia milioni moja wamekimbia makwao kutokana uvamizi wa waasi: IOM

NAIROBI – Zaidi ya raia millioni moja wamekimbia makwao nchini DRC, kutokana uvamizi wa makundi ya watu wenye silaha mashariki mwa taifa hilo

Mkundi ya waasi yamekuwa yakituhumiwa kwa kutekeleza mashabulio dhidi ya raia mashariki ya DRC
Mkundi ya waasi yamekuwa yakituhumiwa kwa kutekeleza mashabulio dhidi ya raia mashariki ya DRC © BADRU KATUMBA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa shirika la kimataifa la kuwashugulikia wahamiaji IOM, ni kwamba raia makundi ya waasi yamesabisha raia hao kumbia, jumala ya raia millioni 6. 1 wakiwa wakimbizi nchini mwao ambapo ni ongezeko la asilimia 17 tangu mwaka uliopita, maeneo ya Kivu mashariki na Ituri yakiathirika zaidi.

Shirika hilo limeongeza kuwa hali hiyo imechangia hali mbaya ya kibinadamu kuendelea kuzorota, raia wakiwa katika hatari ya kukosa chakula na huduma nyingine muhimu, huku raia millioni 26 wakiwa wanahitaji msaada wa dharura.

Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama wa raia mashariki mwa DRC
Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama wa raia mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa

Haya yanajiri wakati huu Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za makosa ya uhalifu wa kivita, ICC, imesema itachunguza tuhuma za utekelezwaji wa vitendo vya uhalifu vilivyofanywa na makundi ya waasi mashariki mwa DRC, kauli inayotolewa siku chache tangu utawala wa Kinshasa na mahakama hiyo zitiliane saini mkataba wa kufanya kazi pamoja.

Kinshasa inawatuhumu waasi wa M23 inaodai wanasaidiwa na Rwanda, kutekeleza uhalifu wakivita mashariki mwa nchi hiyo, tuhuma ambazo hata hivyo Kigali inakanusha.

Jean-Jacques Elakano ni mshauri wa rais Felix tshisekedi akiwa Kinshasa.

“Ulikuwa ni wajibu wa serikali ya Congo kufanya iwezekanavyo iliwahusika waweze kuwasilishwa mbele ya mahakama.’’ alisema Jean-Jacques Elakano ni mshauri wa rais Felix Tshisekedi.

00:44

Jean-Jacques Elakano, mshauri wa rais Felix Tshisekedi

Haya yanajiri baada ya wiki hii shirika la kimataifa la Human Rights Watch, kuchapisha ripoti inayowataja waasi hao kuhusika na vitendo vya mauaji na ubakaji mashariki mwa DRC.

Zaidi ya raia millioni moja wameripotiwa kukimbia makwao nchini humo, kutokana uvamizi wa makundi ya watu wenye silaha mashariki mwa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.