Pata taarifa kuu

Kenyatta kutathmini maendeleo ya mchakato wa amani Goma DRC

Nairobi – Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ambaye ni msimamizi wa mchakato wa amani nchini DRC, anatarajiwa kuwasili mjini Goma mashariki mwa nchi hiyo hivi leo, kutathmini maendeleo ya mchakato huo.

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru Goma mashariki ya DRC kutathmini maendeleo ya mchakato wa usalama
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru Goma mashariki ya DRC kutathmini maendeleo ya mchakato wa usalama © Monicah Mwangi / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta akiwa pamoja na maafisa wa serikali ya DRC, wanatarajiwa kutathmini maendeleo ya mchakato wa amani unaoendelezwa mashariki wa nchi hiyo, ambako makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya jeshi la FARDC na waasi wa M23 bado yanatiliwa shaka.

Ziara ya Kenyatta inakuja wakati ambapo makubaliano ya kusitisha mapigano yameanza kuvunjwa, baada ya kuripotiwa makabiliano kati ya waasi wa M23 na kundi la waasi la Wazalendo ambao wanadai kutetea ardhi ya Congo.

Waasi wa M23 wamekuwa wakisisitiza kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na utawala wa Kinshasa
Waasi wa M23 wamekuwa wakisisitiza kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na utawala wa Kinshasa AFP - GLODY MURHABAZI

Ajenda kuu ya mkutano wa Goma ni pamoja na majadiliano kuhusu kambi ya M23 katika eneo la Rumangabo, jimboni Kivu Kaskazini.

Baada ya karibu miezi mine, jeshi la Congo na M23 wote wameonekana kuwa na misimamo mikali, hali ambayo imezua hofu ya kuzuka tena makabiliano katika majimbo ya Kivu.

Wanajeshi wa Afrika Mashariki na wale ya serikali ya DRC wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi
Wanajeshi wa Afrika Mashariki na wale ya serikali ya DRC wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi AFP - ALEXIS HUGUET

Serikali ya DRC imeendelea kuwashtumu waasi wa M23 kwa kutishia maeneo yao, huku M23 nao wakidai kutotoa ahadi ya kuweka silaha chini, wakati huu pia wakitaka mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.