DRC: Waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa Bosco Ntaganda kulipwa fidia
Nairobi – Mwishoni mwa juma lililopita, majaji katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita, ICC, walithibitisha waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa Bosco Ntaganda nchini CDRC, watalipwa kiasi cha dola za Marekani milioni 30 kama fidia.
Imechapishwa:
Cheza - 00:49
Alifahamika kama “The terminator” Ntaganda alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela mwaka 2019 na mwaka uliopita majaji wa mahakama hiyo waliagiza waathiriwa kulipwa dola milioni 30.
Hata hivyo maagizo hayo hayajaanza kutekelezwa kwa kile mahakama hiyo inasema inanya mapitio kuwabaini waathiriwa halisi wa vitendo vyake.
Mahakama inakadiria kuwa kuna waathiriwa zaidi ya elfu 7 na kwamba kila mmoja anatarajiwa kulipwa dola elfu 4.
Licha ya kuwa Ntaganda, ndio anapaswa kulipa kiasi hicho cha fedha, mahakama ilibaini uwa hana uwezo na badala yake kiasi hicho kitalipwa kutoka kwenye mfuko maalumu wa mahakama hiyo ya the hague.