Pata taarifa kuu

Mauaji ya halaiki Rwanda: Majaji wa UN waunga mkono kuachiliwa kwa Kabuga

Je, Félicien Kabuga atakuwa huru hivi karibuni? Mahakama ya Rufaa ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kesi ya mfanyabiashara huyo wa Rwanda iliamuru, Jumatatu, Agosti 7, kusimamishwa kwa "muda usiojulikana" wa kesi hiyo na kuwataka majaji wa mahakama hiyo kupitia upya kuzuiliwa kwake kwa muda. Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu, Félicien Kabuga alikamatwa katika vitongoji vya Paris mnamo mwezi Mei 2020.

Félicien Kabuga, 88, (anadai kuwa na miaka 90), yuko katika hali mbaya ya afya. Mnamo Juni 6, majaji walimtangaza kuwa "hafai" kujibu mashtaka.
Félicien Kabuga, 88, (anadai kuwa na miaka 90), yuko katika hali mbaya ya afya. Mnamo Juni 6, majaji walimtangaza kuwa "hafai" kujibu mashtaka. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa bado haujafunga kabisa kesi ya mfanyabiashara huyo wa zamani. Félicien Kabuga hajakuwa huru kabisa. Anabaki chini ya mamlaka ya mahakama. Majaji wa mahakama hiyo sasa watatathmini mustakabali wake. Wanatarajia kuamua juu ya kuachiliwa kwa dhamana. Kwa hivyo haionekani kabisa iwapo Félicien Kabuga atapita kwa miguu, Jumatano, Agosti 9, milango ya gereza la Scheveningen, ambako anaishi kwa zaidi ya miaka mitatu.

Pengine hatarejeshwa huko Asnières-sur-Seine, katika viunga vya Paris, ambako alikamatwa mwezi Mei 2020. Baadhi ya watoto 13 wa mfanyabiashara huyo wanapatikana nchini Ufaransa, Uingereza na Ubelgiji hasa. Kuna uwezekano mkubwa kwamba majaji wataamuru apewe hifadhi katika moja ya nchi hizi tatu, ambayo itakuwa na wajibu wa kushirikiana nao.

Mtu huyo anachukuliwa kuwa "mfadhili" wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambayo yasababisha vifo vya takriban watu 800,000 mwaka 1994. Alikamatwa nchini Ufaransa mwaka 2020 chini ya utambulisho wa uongo, alikuwa akisakwa kwa miaka 25 na mahakama ya kimataifa.

Félicien Kabuga, 88, (anadai kuwa na miaka 90), yuko katika hali mbaya ya afya. Mnamo Juni 6, majaji walimtangaza kuwa "hafai" kujibu mashtaka. Hata hivyo walikuwa wameweka utaratibu maalum ambao haujawahi kushuhudiwa, wakisema wanataka "kuchangia katika kudumisha amani nchini Rwanda".

Ni utaratibu huu uliorahisishwa ndio unaowapa motisha majaji wa Mahakaam ya Rufaa; wanaamini kwamba mahakama maalum ya uhalifu wa kivita ilifanya "kosa la kisheria" kwa uamuzi huu, na kwamba "kusimamishwa kwa muda usiojulikana kwa kesi" kunapaswa kuchukuliwa "kutokana na kutoweza kwa Félicien Kabuga kusimama mbele ya majaji kujibu mashitaka yanayomkabili kwa anatatizo la akili".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.