Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Watatu wauawa katika shambulizi jipya linalohusishwa na ADF nchini Uganda

Mwanamke mmoja mzee na watoto wawili waliangamia katika kisa cha moto baada ya nyuma yao kuteketezwa kwa moto siku ya Jumatatu, kitendo kilichofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) kundi lenye mafungamano na kundi la Islamic State katika kijiji kimoja magharibi mwa Uganda, mamlaka katika eneo hilo imesema siku ya Jumanne.

Moja ya operesheni ya pamoja kati ya majeshi ya Uganda na DRC katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga nchini DRC, Desemba 14, 2021.
Moja ya operesheni ya pamoja kati ya majeshi ya Uganda na DRC katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga nchini DRC, Desemba 14, 2021. © SEBASTIEN KITSA MUSAYI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha mbali katika wilaya ya Kamwenge, eneo lililokumbwa na shambulio, wiki moja mapema lililohusishwa na ADF na ambapo wanakijiji kumi waliuawa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Kamwenge, Isiah Byarugaba, akihojiwa na shirika la habari la AFP, washambuliaji hao walichoma moto nyumba walimokuwa wahanga hao.

"Waasi wa ADF waliwaua watu watatu, mwanamke mzee na wajukuu wake wawili. Walichomwa hadi kufa katika nyumba yao jana usiku," amesema. Jeshi na polisi waliwafuata waasi hao, ameongeza. "Tuko tayari kutathmini hali na kuhamasisha jamii ya eneo hilo kuzuia mashambulizi ya kikatili ya magaidi wa ADF dhidi ya raia wasio na hatia," amesema.

Waasi wa Uganda, ADF, wengi wao wakiwa Waislamu wamekuwa wanaendesha harakati zao tangu katikati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambapo wameua maelfu ya raia. Mnamo mwaka wa 2019, walitangaza kujiunga na kundi la ISIS, ambayo sasa inakiri kuhusika na baadhi ya vitendo vya na kusema kuwa ADF ni kitengo chao "katika Afrika ya Kati".

Mto Tako, mpaka wa asili kati ya Uganda na DRC, ni eneo la zamani la kivuko cha ADF.
Mto Tako, mpaka wa asili kati ya Uganda na DRC, ni eneo la zamani la kivuko cha ADF. © Lucie Mouillaud / RFI

Uganda na DRC zilianzisha mashambulizi ya pamoja mwaka 2021 kuwafukuza ADF kutoka ngome zao za Kongo, na kushindwa hadi sasa kukomesha mashambulizi ya kundi hilo. Mnamo mwezi wa Oktoba, watalii wawili, mwanamume wa Uingereza na mwanamke wa Afrika Kusini, pamoja na Mwelekezaji wao, waliuawa katika mbuga ya Queen Elizabeth Park (magharibi), katika shambulio lililodaiwa na kundi la Islamic State.

Mwezi Juni, watu 42, wakiwemo wanafunzi 37, waliuawa katika shule ya upili magharibi mwa Uganda katika shambulio ambalo pia lilihusishwa na ADF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.