Pata taarifa kuu

Mwanaharakati wa LGBTQ adungwa kisu nchini Uganda

Mwanaharakati mashuhuri wa jamii ya wapenzi wa jinsi moja ,LGBTQ, nchini Uganda alidungwa kisu siku ya Jumatano na watu wasiojulikana kwenye pikipiki alipokuwa akiendesha kuelekea kazini, polisi na mwanaharakati wa haki za binadamu wamesema.

Steven Kabuye, ambaye anatetea vijana wa LGBTQ, aliwaambia wachunguzi kwamba amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa tangu mwezi Machi 2023.
Steven Kabuye, ambaye anatetea vijana wa LGBTQ, aliwaambia wachunguzi kwamba amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa tangu mwezi Machi 2023. © AP
Matangazo ya kibiashara

Steven Kabuye, 25, alijeruhiwa na kuachwa akidhaniwa kuwa amekufa wakati wa shambulio hilo lililotokea katika viunga vya mji mkuu Kampala, kabla ya kuokolewa na wakaazi, polisi imesema. Wanaharakati wa haki za binadamu tayari wameonya juu ya hatari ya mashambulizi dhidi ya watu wa jumuiya ya wapenzi wa jinsi moja, LGBTQ, nchini Uganda baada ya nchi hiyo kupitisha mojawapo ya sheria kali zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja duniani mwaka jana.

Msemaji wa polisi, Patrick Onyango, amesema: "Kulingana na Bw. Kabuye, watu wawili waliovalia kofia ya pikipiki wakiwa kwenye pikipiki walmkaribia. Abiria huyo alimvamia akilenga shingoni kwa kisu," amesema Bw Onyango. "Washambuliaji walimfuata na kumchoma kisu tumboni, kabla ya kumwacha wakidhania kuwa amekufa," ameongeza, akibainisha kuwa wakazi wa mtaa huo walimuokoa na kumpeleka hospitalini. Kulingana na msemaji wa polisi, mwathiriwa huyo anaendelea vizuri.

Bw. Kabuye, ambaye anafanya kazi katika Wakfu wa Colored Voices Media, ambao unatetea vijana wa LGBTQ, aliwaambia wachunguzi waliomtembelea hospitalini kwake kwamba amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa tangu mwezi Machi 2023.

Mnamo mwezi Mei 2022, Uganda ilipitisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsi moja ambayo ni pamoja na vifungu vinavyofanya "ushoga uliokithiri" kuwa ni kosa linaloadhibiwa kwa kifo na hadi kifungo cha maisha jela kwa uhusiano wa kimaadili kati ya watu wa jinsia moja. Sheria hii ililaaniwa na watetezi wa haki za binadamu na nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.