Pata taarifa kuu

Watatu wafariki na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa kufuatia moto mkubwa uliotokea jijini Nairobi

Takriban watu watatu wamefariki na wengine 271 kujeruhiwa katika moto mkubwa uliosababishwa na mlipuko wa gesi usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa mjini Nairobi, naibu inspekta jenerali wa polisi wa Kenya amesema siku ya Ijumaa.

Karibia watu watatu wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo wa usiku wa kuamkia leo
Karibia watu watatu wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo wa usiku wa kuamkia leo REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

 

Baada ya saa kadhaa, moto huo, ambao ulizuka usiku wa manane, huku maafisa wengi wa kikosi cha Zima moto wakitumwa katika eneo la tukio, ulidhibitiwa mwendo wa saa 3:00 asubuhi, walibaini waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Lori "lililojaa gesi lililipuka, na kusababisha moto mkubwa ambao ulienea haraka" huko Embakasi, wilaya ya mji mkuu wa Kenya, msemaji wa serikali Isaac Maigua amesema kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Moto huo "uliharibu magari na mali kadhaa za biashara, zikiwemo biashara nyingi ndogo na za kati. Kwa bahati mbaya, nyumba za makazi katika eneo hilo pia ziliteketea, na idadi kubwa ya wakazi walikuwa bado wakiwa ndani kwani ilikuwa usiku," amesema Isaac Maigua Mwaura.

Wito umetolewa kwa raia wa Nairobi kutoa damu kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika kwenye makasa huo.
Wito umetolewa kwa raia wa Nairobi kutoa damu kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika kwenye makasa huo. REUTERS - MONICAH MWANGI

"Takriban watu 271 wamelazwa katika hospitali mbalimbali jijini Nairobi na...watu watatu wamefariki," Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, aliyezuru eneo la tukio, ameambia wanahabari. Hapo awali, serikali ilisema watu 222 walijeruhiwa na wengine wawili kufariki.

"Tulikuwa ndani ya nyumba na tukasikia mlipuko mkubwa," James Ngoge, ambaye anaishi mkabala na mahali moto ulipotokea, ameliambia shirika la habari la AFP. "Jengo lote lilitikiswa na tetemeko kubwa, tulihisi kama litaanguka. Mwanzoni hata hatukujua nini kilikuwa kinatokea, ilikuwa kama tetemeko la ardhi. Mimi ni nafanya biashara barabarani ambayo iliharibiwa kabisa," ameongeza.

"Tulisikia kwanza kitu kama mlipuko mkubwa ambao ulifuatiwa kwa haraka na mwingine mkubwa zaidi. Ni wakati huu ambao nyumba yetu ilitikisika sana na dirisha likaanguka na kupasuka," amesema Felix Kirwa, mkazi wa kitongoji hicho na mwendesha pikipiki za kukodiwa (boda-boda).

Rais Ruto ameagiza waliohusika na kutoa leseni kwa kituo hicho kushtakiwa
Rais Ruto ameagiza waliohusika na kutoa leseni kwa kituo hicho kushtakiwa REUTERS - THOMAS MUKOYA

“Hapo ndipo tulikimbia pande tofauti, nilimshika mdogo wangu na kukimbia naye, sikujua watoto wengine wawili walikuwa wamekimbilia wapi hadi leo asubuhi nilipowachukua, wapo na wako salama salimini, lakini nina jeraha mguuni na nilifungwa bandeji lakini niko sawa,” anabaini.

Mnamo mwezi Juni 2018, takriban watu 15 waliuawa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa katika moto uliotokea katika soko kubwa zaidi la kiahari la Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.