Uganda: Mahakama ya ICC yatoa fidia kwa waathiriwa wa vitendo vya waasi wa LRA
Nairobi – Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita imetoa malipo ya fidia kwa waathiriwa katika kesi inayomhusisha kamanda wa zamani wa waasi wa Lord's Resistance Army, Dominic Ongwen, ambaye sasa amefungwa.
Imechapishwa:
Cheza - 01:03
Ongwen alikuwa kamanda mkuu wa LRA, wanamgambo wa waasi waliokuwa wakiendesha shughuli zao kaskazini mwa Uganda kutoka 1987 kwa miongo miwili.
Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ya (ICC) ilimtunuku kila mwathiriwa, ambao idadi yao inakadiriwa kuwa 49,772, fidia ya Dola 800 za Marekani kila mmoja.
Hii ni rekodi ya $56 milioni kwa jumla, lakini waathiriwa hawatalipwa mara moja.
Baraza la uaminifu lilipewa jukumu la kukusanya pesa zinazohitajika kwa ajili ya fidia, huku jumuiya ya kimataifa ikialikwa kutoa michango. Mahakama pia ilitoa malipo ya pamoja kwa jamii.
Hizi zitazingatia mipango ya ukarabati inayolenga kurekebisha aina zote za uharibifu uliopatikana.
Dominic Ongwen alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita 61 na uhalifu dhidi ya ubinadamu na ICC mnamo Februari 2021.Uhalifu uliofanywa kati ya 2002 na 2005 ulijumuisha uhalifu wa kingono na kijinsia. Alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.
Kamanda huyo wa zamani wa LRA alishiriki katika vita vilivyosababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kuwaacha mamia wakiwa wameuawa kaskazini mwa Uganda. Kwa sasa Ongwen anatumikia kifungo chake jela nchini Norway.