EAC yakanusha madai ya kuzinduliwa kwa sarafu ya pamoja
Nairobi – Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imekanusha kutoa chapisho kwenye mtandao wa kijalii wa X, kuwa nchi wanachama zimezindua sarafu.
Imechapishwa:
Tangazo hili la EAC yenye makao yake jijini Arusha nchini Tanzania, limekuja baada ya kuwepo kwa chapisho mwishoni mwa wiki iliyopita, kwenye ukura wa X uliokuwa na jina la Government of East Africa.
The EAC Secretariat wishes to inform all our stakeholders that the Partner States' journey to a single currency is still a work in progress. Kindly ignore any rumours circulating in social media on the unveiling of new banknotes for the region. pic.twitter.com/kunhBtzpuK
— East African Community (@jumuiya) March 3, 2024
Kwa mujibu wa taarifa kwenye akaunti hiyo ghusi, sarafu hiyo ya pamoja imepewa jina la East African Sheafra, ikijumuisha shilling ya Afrika Mashariki na Franca kutoka nchi za Rwanda, Burundi na DRC.
Akaunti pia ilichapisha picha ya noti bandia ya sarafu moja inayodaiwa kuwa kwenye mchakato wa kuzinduliwa.
Chapisho hili limepokea maoni zaidi ya Laki Tano, na lilisambazwa na baadhi ya vyombo vya habari na watu maarufu mtandaoni katika ukanda wa Afrika Mashariki.
EAC ilitupilia mbali ripoti ya kuwepo kwa sarafu ya kanda ya pamoja siku hiyo ya Jumapili, ikisema kwamba mchakato wa kuundwa kwa sarafu ya pamoja bado unaendelea.
Mwaka 2013, nchi wanachama wa EAC ziliahidi kuzindua sarafu ya pamoja kufikia 2024 lakini mpango huo umeahirishwa hadi 2031.