Pata taarifa kuu

Uganda: Tahadhari imetolewa baada ya waasi wa ADF kuvuka mpaka

Nairobi – Usalama umeimarishwa nchini Uganda, baada ya vyombo vya usalama kudai waasi wa ADF wanalenga kutekelza mashambulio kwenye miji mikuu ya nchi hiyo.

Waasi wa ADF wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika mpaka wa Uganda na DRC.
Waasi wa ADF wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika mpaka wa Uganda na DRC. © FMM
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya usalama nchini Uganda vimesema wapiganaji wa ADF wenye uhusiano na kundi la kigaidi la ADF, waliingia nchini Uganda kutoka DRC mwishoni mwa juma na wanalenga kutekeleza mashambulio nchini humo kwenye nyumba za ibada, shule na kwenye mikutano ya hadhara, polisi wakitaka raia kuchukuwa tahadhari.

Mwaka 2021 jeshi la Uganda na DRC lilianzisha operesheni ya pamoja dhidi ya ADF, lakini operesheni hiyo imekosa kuzaa matunda hadi sasa, licha ya rais Museveni kusisitiza kwamba operesheni hiyo imezaa matunda baada ya kuuawa kwa makamanda wakuu wa ADF.

Kundi la waasi limekuwa litekeleza mashambulio nchini Uganda hasa eneo la magharibi, ambapo mwezi Juni mwaka uliopita mamia ya wanafunzi waliuawa, mwezi oktoba mwaka uliopita kundi hilo likihusishwa na mauwaji ya watali wawili.

ADF lenya chimbuko lake nchini Uganda miaka ya 90, lilikimbilia nchini DRC baada ya jeshi la Uganda kufaulu kulithibiti, ambapo kundi hilo lilikuwa likilalamikia namna serikali ilikuwa ikiwabagua waumini wa dini ya Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.