Pata taarifa kuu
KENYA-IEBC-SIASA

IEBC yafutilia mbali madai ya upinzani

Tume ya uchaguzi nchini Kenya inasisitiza kuwa haitaondoka madarakani kupitia maandamano ya upinzani.

Mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Mji mkuu wa Kenya Nairobi. Reuters/Noor Khamis/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo Isaak Hassan akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge inayoshughulia maswala ya sheria na haki jijini Nairobi, amewatetea Makamishena wenzake na kusema wamefaya kazi nzuri kuelekea uchaguzi Mkuu ujao na wanalindwa na Katiba.

Aidha, amewataka wanasiasa kuelewana kwanza, kabla ya kuitaka Tume hiyo kujiuzulu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Samuel Chepkonga ametoa wito kwa Makamishena hao kutoa nafasi ya mazungumzo ili mwafaka upatikane kutoka kwa wadau mbalimbali nchini humo.

Kwa upande wao, viongozi wa upinzani wakiomgozwa na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga wanasisitiza kuwa wataendelea na maandamano kila Jumatatu kuwashinikiza Makamishena hao kujizulu kwa tuhma za ufisadi na kuipendelea serikali, madai ambayo tume hiyo inakataa.

Hayo yakijiri polisi nchini Kenya wameangiza uchunguzi wa ndani kubaini maafisa wa polisi waliotumia nguvu kupita kiasi kuwapiga waandamanaji wa upinzani hapo jana jijini Nairobi wakati wa maandamano ya upinzani dhidi ya Makamishena wa Tume ya Uchaguzi.

Inspekta wa polisi Joseph Boinnet ameshtumu polisi waliotumia nguvu huku ripoti zikisema mwandamanaji aliyepigwa na maafisa wa tatu kwa mpigo, amepoteza maisha.

Mamlaka inayothathmi utendaji wa polisi nchini humo IPOA imesema itamfungulia mashtaka ya mauaji afisa wa polisi waliotumia nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.