Pata taarifa kuu
KENYA -SUDANI

Rais Uhuru Kenyatta awasili Sudani kwa ziara ya siku mbili

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta yumo nchini Sudani kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kwa mwaliko wa rais wa Sudan Omar Al Bashir, Siku kadhaa baada ya rais Bashir kutoa wito kwa nchi za Afrika kujiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto), akiwa na mwenyeji wake Rais wa Sudan, Omar Bashir, 29 October 2016.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto), akiwa na mwenyeji wake Rais wa Sudan, Omar Bashir, 29 October 2016. Kenya State House
Matangazo ya kibiashara

Marais Al Bashir na Uhuru Kenyatta watajadili masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja na njia za kukuza mahusiano baina ya nchi hizo,imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Sudan.

Aidha wakati wa ziara hiyo nchi hizo mbili zitatiliana saini idadi kadhaa ya mikataba ya makubaliano na ushirikiano baina ya nchi hizo katika sekta ya vyombo vya habari, utamaduni na elimu ya juu, teknolojia, ujenzi na makazi, na kilimo na ufugaji.

Mbali na mikataba ya ushirikiano baina ya nchi hizo, Rais Kenyatta na mwenyeji wake wanatarajia kujadili suala la uwezekano wa kujiondoa kwenye mahakama ya ICC ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Kamal Ismail amesema ziara ya rais Kenyatta imekuja wakati muhimu.

Kufuatia tangazo la Afrika kusini kuamua kujiondoa katika mahakama ya ICC Juma lililopita, Sudani imewataka wanachama wa ICC barani Afrika kujiondoa katika mahakama hiyo kwa madai kuwa ni chombo cha kikoloni kinachotumika dhidi ya waafrika .
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.