Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-GAZA

Uingereza, Ufaransa, Denmark na Sweden zaongeza shinikizo zaidi kwa Serikali ya Israel

Nchi ya Marekani na zile za Ulaya zimeendelea kuongeza shinikizo zaidi kwa nchi ya Israel kuhusiana na mpango wake wa kuendelea makazi ya kudumu zaidi ya elfu 3 kwenye eneo la ukanda wa gaza ambalo linamgogoro.

Nyumba ambazo ni miongoni mwa majengo mapya yanayoendelezwa na Serikali ya Israel kwenye ukanda wa Jerusalem
Nyumba ambazo ni miongoni mwa majengo mapya yanayoendelezwa na Serikali ya Israel kwenye ukanda wa Jerusalem Reuters
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani iliitaka Serikali ya Israel kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka kuendelea na ujenzi wa makazi ya kudumu kwenye eneo la walowezi wa Kipalestina.

Safari hii shinikizo zaidi limeongezeka kwa nchi ya Israel baada ya mataifa ya Uingereza, Sweeden, Uhispani, Ufaransa na Denmark kuitaka nchi hiyo kuachana na mpango wake huo kwakuwa utachangia kuzorotesha hali ya usalama kwenye eneo hilo.

Siku ya Jumatatau katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon alionesha wasiwasi wake kuhusu mpango wa Israel kuendelea makazi ya kudumu kwenye eneo la ukanda wa Gaza.

Katika taarifa yake Ban amesema kuwa Israel kuendelea na mpango wake kutasababisha kuchelewesha kupatikana kwa amani kwenye eneo hilo hasa kati yake na Palestina.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza mpango wa serikali yake kuanza tena ujenzi wa makazi ya kudumu kwenye ukanda wa Gaza siku ya alhamisi hatua iliyokuja saa chache baada ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio kuitambua Mamlaka ya Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.