Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINE

UN yazitaka Israel na Palestina kurejea kwenye meza ya mazungumzo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon amezungumza kwa nyakati tofauti na viongozi wa Israel pamoja na mamlaka ya Palestina na kuwashawishi kurejea kwenye meza ya mzungumzo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akisihi Israeli na Palestina kuketi kwenye meza ya mazungumzo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akisihi Israeli na Palestina kuketi kwenye meza ya mazungumzo. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku mbili mfululizo, katibu mkuu Ban amezungumza na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kujaribu kumshawishi kurejea kwenye meza ya mazungumzo pamoja na kulegeza masharti ya kufanya mazungumzo na mamlaka ya Palestina.

Ban Ki Moon amerejelea kauli yake kwa rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas ambaye amemueleza kuguswa na namna ambavyo mzozo huo unaelekea na kwamba huenda kusiwe na suluhu kabisa.

Hatua ya Ban ki Moon kuingilia kati mzozo kati ya Palestina na Israel, inakuja ikiwa zimepita siku chache toka waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry akiri kuwa nchi yake inakabiliwa na wakati mgumu wa kuzishawishi pande hizo kuwa na mazungumzo ya kusaka suluhu.

Hivi karibuni utawala wa Palestina ulitia saini mkataba unaotoa nafasi kwa nchi hiyo kutafuta uungwaji mkono zaidi na taasisi za Umoja wa Mataifa hatua iliyojibiwa na Israel kwa kutangaza kusitisha mawasiliano ya kidiplomasia na nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.