Pata taarifa kuu
UTURUKI-Ajali

Uturuki yatangaza maombolezo ya kitaifa

Uturuki imekumbwa na tukio baya ambalo halijawahi kutokea katika historia ya taifa hilo kwa kipindi cha miongo miwili. Watu 230 wamefariki katika ajali ya moto iliyotokea jana jumanne katika eneo la Soma, baada ya mgodi wa makaa ya mawe kushambuliwa na moto.

Ajali iliyotokea kwenye machimbo ya mkaa wa mawe katika nji wa Soma, nchini Uturuki, Mei 14 2014.
Ajali iliyotokea kwenye machimbo ya mkaa wa mawe katika nji wa Soma, nchini Uturuki, Mei 14 2014. REUTERS/ Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

β€œMatumaini ya kuwapata manusura yamekua ndoto”, amesema waziri wa nishati Taner Yildiz.

Ajali hii imetokea jana mashariki mwa Uturuki, na huenda idadi ya watu 230 waliyofariki ikaongezeka.

Waziri Taner Yildiz, amesema ni vigumu kuwapata manusura, kwani bado moto unaendelea kushambulia mgodi huo unaopatikana katika mkoa wa Manisa.

Mmoja kati ya wachimba migodi ambaye amenusurika katika ajali iliyotokea kwenye machimbo ya mkaa wa mawe katika mkoa Soma Komur, magharibi mwa Uturuki,  Mei 12 mwaka 2014..
Mmoja kati ya wachimba migodi ambaye amenusurika katika ajali iliyotokea kwenye machimbo ya mkaa wa mawe katika mkoa Soma Komur, magharibi mwa Uturuki, Mei 12 mwaka 2014.. REUTERS/Osman Orsal

Hata hivo shirika la habari la serikali limearifu mapema leo asubuhi kwamba watu sita wameokolewa wakiwa hai, bila hata hivo kutoa maelezo zaidi kuhusu afya yao.

Mapema jioni jana jumanne,waziri Yildiz alisema kwamba wachimba migodi 363 waliokolewa baada ya tukio hilo.

Kulingana na taarifa ziliyotolewa na viongozi, wachimba migodi 787 walikua ndani ya machimbo hayo ya makaa ya mawe wakati mlipuko na moto vilipotokea jana alaasiri.

β€œIdadi ya watu waliofariki inaendelea kuongezeka, jambo ambalo linatia hofu. Kama kuna uzembe umetokea, hatutoendelea kukaa kimya, tunapaswa kuchukua hatua zinazo hitajika kisheria”, amesema waziri Yildiz.

Watu 80 wamejeruhiwa, wakiwemo wanne ambao wako katika hali mahututi.

Idadi kubwa ya askari polisi imepelekwa kwenye eneo la tukio ili kurahisisha shughuli za uokozi kwa kuwasafirisha majeruhi kwenye hospiali ya Soma, mji ambako mgodi huo unapatikana.

Ndugu na marafiki wa wachimba migodi wakisubiri kuona miili ya ndugu zao kwenye hospiali ya Soma.
Ndugu na marafiki wa wachimba migodi wakisubiri kuona miili ya ndugu zao kwenye hospiali ya Soma. REUTERS/Ihlas/Yilmaz Saripinar

Tayari Uturuki imetangaza siku tatu ya maombolezo ya kitaifa baada ya ajali hio iliyosababisha vifo vya watu 230, kwa mujibu wa tathmini ya awali, imetangaza ofisi ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan.

"Kutokana na maafa yaliyosababishwa na ajali iliyotokea katika mji wa Soma kwenye mgodi wa makaa ya mawe, serikali imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu tangu (Jumanne) Mei 13," ilisema taarifa hiyo.

Milipuko katika migodi imekua ikitokea mara kwa mara nchini Uturuki, hususan katika sekta ya kibinafsi, ambako tahadhari za kiusalama haziheshimishwe.

Ajali mbaya ambayo iliwahi kutokea nchini Uturuki ni ile iliyotokea mwaka 1992 katika mgodi wa gesi ya Zonguldak kaskazini mwa Uturuki iliyosababisha vifo vya watu 263.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.