Pata taarifa kuu
UMOJA WA MATAIFA-PALESTINA-ISRAELI-Usalama

UN inatiwa wasiwasi na hali inaendelea Gaza

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutakana katika kikao cha dharura leo Alhamisi kuzungumzia mashambulizi kati ya jeshi la Israel na kundi la Kislamu la Hamas katika ukanda wa Gaza.

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel katika Uganda wa.
Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel katika Uganda wa. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israeli likiendesha mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israeli likiendesha mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza. AFP/JACK GUEZ

Jeshi la Israel limetekeleza mashambulizi zaidi katika ukanda wa Gaza na kusabibisha vifo vya zaidi ya watu 70 na zaidi ya 500 kujeruhiwa.

Israel inasema, kundi la Hamas limerusha zaidi ya maroketi 200 katika ardhi yake huku mengine yakifika mjini Tel Aviv.

Mwakilishi wa Mamlaka ya Palestina, Riyadh Mansour ameishtumu Israel kuwaua raia wake na kutaka Baraza la Usalama kuchukua hatua zinazohitajika.

Matamshi hayo yamemkera Balozi wa Israel katika Umoja huo wa Mataifa Ron Prosor.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa Israel na Palestina kumaliza tofauti zao na kusitisha mashambulizi.

Wakati huo huo kamati ya Jumuiya mataifa ya kislamu inakutana hii leo ili kujadili kuhusu mashambulizi hayo ya Israeli nchini katika mji wa Gaza, nchini Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.